Naomba kuulia, hii Echo-Aid ni kampuni halali?

dalbega

Member
Apr 13, 2012
99
32
Mke wangu aliomba nafasi ya kazi iliyokuwa posted kwenye mtandao wa zoomtanzania.com. Ilikuwa inatangazwa na echo-aid (Echo Aid Fund – Humanitarian Assistance). Kwenye zoom walisema wapo based Dar lakini baadae wakaonyesha wapo Mwanza. Walimwandikia mail kwamba wamemshortlist, lakini ni lazima afanya mtihani wa TST ambao anaweza kuupata either www.novran.com au www.frillhr.net.

Aliufanya na akatuma matokeo lakini mpaka sasa hawajamjibu chochote. Mwenye taarifa tafadhali aseme kama hawa watu ni genuine au ni matapeli, kwa sababu mtihani ulikuwa wa kulipia dola 120. Asante
 
Mkuu siku nyingine kuwa makini sana. Tena mwambie na mkeo awe makini kuhusu matumizi ya hii mitandao.
Kazi yoyote legitimate duniani hakuna employer atakaye omba pesa kutoka kwa muomba kazi. Ukiona tangazo la kazi lime husisha masuala ya kutoa pesa kimbia sana na wala usiangalie nyuma. Pole sana mkuu. hao matapeli. Tena angalia kama alilipa kwa credit card pia awe makini wataalamu huwa wanazimanipulate na kutoa pesa ki ulaini sana.
 
Back
Top Bottom