Naomba kutoa hoja, "mikataba yote iwe kwenye lugha yetu"

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,121
2,064
Hawa tunaowaita wataalam wetu kimsingi wanatumia tatizo la lugha kuficha uovu wao kwenye mikataba huku wao wakipokea mafao yao kupitia mgongo wa nyuma.

Kulikomesha hili, inatakiwa mikataba yote iandikwe kwa lugha ya Kiswahili ili hata yule ambaye hajui kiingereza aelewe maudhui ya mikataba insyosainiwa.

Mara nyingi hii mikataba inasainiwa kwa mbwembwe nyingi sana. Kumbe ndani yake kuna uovu unafichwa huku wachache wakinufaika.

Mh. /rais /Dr JPM anatakiwa kulifanyia kazi hili. Hii nchi ni ya watanzania wote. Hata wasiojua Kiingereza au Lugha nyingine za nje wana haki ya kujua maudhui ya mikataba inayosainiwa ili kama hawakubaliani wapate ujasiri wa kuipinga.

Leo hii kuna utata wa kisheria dhidi ya makontena ya mchanga. Mali tunaibiwa sisi, eti kesi wafungue wao!!!!!! Huu ni uboya wa kimataifa unaotaka kufanywa na ACACIA.

Watanzania tumuunge mkono Rais wetu kwa hili na wote waliohusika kuanzia kwa B. W. MKAPA, J. M. KIKWETE wawajibishwe effectively maana hakuna namna. Hili likifanyika MAGU atajijengea heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania.
 
"bila kuathiri masharti ya ibara ya tatu hapo juu,fasihi ya nne,afisa ugani anaweza kutoa kibali baada ya kushauriana na afisa vileo kuhusu masharti ya leseni kama yanavyoelezwa kwenye sheria ya nyumba za starehe"

lusinde ataelewa nini hapo hata ukiandika kwa kigogo!!!!
 
Hilo silo tatizo pasi na shaka., Tatizo ni mfumo mbovu alouanzisha Mkapa enzi izoooo...!! Ka Nyerere hakakua kapumbavu kalivosema hatujakomaa bado kuruhusu madini kuchimbwa...!!!
17273018837085578483
 
issue sio lugha tu, bali critical and analytical thinking.

Tatizo hapa ni chenga ambazo hawa tunaowaita wasomi hutuingiza kwa kufanya mambo ya msingi kwa njia ya voda faster. Wanajua wazi kuwa wananchi walio wengi hawaelewi kinachoendelea hivyo hutumia mwanya huo kujifanya kuwa wanasaidia nchi kumbe ndo wanaiangamiza. Mikataba yote na sheria zilizopitishwa kwa mfumo wa voda faster zinatakiwa kuwa reviewed na wote waliokuwa chanzo cha kutufikisha hapa tulipo wawajibishwe bila kuangalia sura /title zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom