Naomba kujuzwa zaidi kuhusu gari aina ya Mazda RX 8

TADPOLE

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
2,800
9,041
Wadau habari,

Mwezi uliopita kupitia STB JAPAN niliweza kuagiza gari tajwa kwenye tittle from abroad bahati nzuri imefika ipo bandarini so kuanzia this week ntaishughulikia malipo yote bandarini na hatimaye iwe mikononi mwangu by this week.

Kikubwa nilichoipendea hii gari ni muonekano wako unakufanya unakuwa comfortable na kingine nilitaka nibadilishe ladha baada ya kutumia Toyota kwa miaka mingi sana.

Sasa ninachotaka tushirikiane kuhusu gari hizi ni changamoto zake ikiwepo ubora wa injini yake,upatikanaji wa spare Tanzania (nilinunua bila kuangalia hilo), utumiaji wake wa mafuta na kadhalika.
Taarifa za gari

Engine capacity cc 1950
Year 2004...
RHD,2doors,4seats,AT
Mileage 96000.


IMG-20191023-WA0026.jpeg
IMG-20191023-WA0031.jpeg
IMG-20191023-WA0024.jpeg
IMG-20191023-WA0027.jpeg
 
Tatizo la hii gari ni engine yake. Tegemea siku moja unaipaki mahali na ukiwasha ndio haiwaki tena. Engine yake inahitaji umakini wa hali ya juu sana maana inatumia rotary engine. Kuna mada humu ilishajadili sana hiyo gari
dah mkuu huo uzi ulikua na tittle gani?.labda naweza kupata more information huko rotary engine zinakuwaga na changamoto sana yaani
 
Inaonesha wapenda mbio
Yeah hii gari subaru,Altezza zote haziingizi mguu sema ndio hivyo una changanoto nyingi kumbe hasa muundo wa injino yake rotary engine..injini hizi kumbe kila baada ya 100k unatakiwa uibadilishe na pia fuel consumption nasikia ni kubwa kwa kweli 1 kilometer zinakatika lita 8 za petrol imagine.
 
Yeah hii gari subaru,Altezza zote haziingizi mguu sema ndio hivyo una changanoto nyingi kumbe hasa muundo wa injino yake rotary engine..injini hizi kumbe kila baada ya 100k unatakiwa uibadilishe na pia fuel consumption nasikia ni kubwa kwa kweli 1 kilometer zinakatika lita 8 za petrol imagine.
Mkuu utarudisha japan au utafanyeje!?
 
Niliwahi kuandika humu khs hio mazda rx-8,ngoja ni-paste tena hapa.

Tribute to my mazda rx-8.

Nilikua na mazda rx-8 nikaipimp ikawa ya "kitozi"hatariiiii, balaa lake inakula engine oil si mchezo.

Ni cc 1300 tu,yangu ilikua ni manual 6 speed, horsepower inatoa 240,nilikua nikitembea road hakuna cha tezza sijui nini labda subaru baadhi ndo zilikua zinanisumbua tena mostly STI WRX.

Barabarani ina balance balaa(weight distribution) ni 50% kwa 50%(wenye uelewa wa magari wataelewa hii).

Consumption yake ni lita 1 kwa km 6-8 wkt ni cc 1300 tu, kutegemeana na uendeshaji wangu,hahah.

Ikifika km 100,000 engine overhauling inaweza kuhusika,niliiuza ikiwa na km 75,000 kwa mhindi lkn mpk sasa iko barabarani na zaidi ya km 100,000 na inadunda bila matatizo yoyote yale.

So kwenye rotary engine haitakiwi gari asubuh kuiwasha na kuondoka hapohapo unaiacha kwanza inachemka then ndo unaondoka na ukija kuipaki usiizime pia hapohapo. Na ili idumu atleast kila siku lazima uhakikashe gari inakimbizwa(rev)mpk mshale ufike kwenye redline, kwangu ilikua ni rpm 9000 ukifanya hivyo inadumu

Next challenge nataka 1997 Manual mazda rx-7(Najua matatizo ya hio gari lkn ndo hivyo tena naitaka hivyo hivyo)

I'll miss u my mazda rx-8.
 
Kwanza hongera kwa kuvuta chombo ilhali sisi wengine san-lg tu zinatuoa shida.

Niliwahi kuona uzi wakizongelea hizo gari na changamoto yake ya engine, kiukweli inakatisha tamaa., pia niliwahi pia mtaa mmoja kariakoo nikakuta kama 4 hivi zimepark zimekufa nikaanza kuamini ya huo uzi.

Cha msingi matunzo tu, zingatia matunzo na service kama dozi ya ARV
 
Mkuu, kwanza kilicho nileta hapa ni kukupongeza kwa kumiliki mkoko in town.

Na kwakuwa sina la kukushauri, basi ebu agiza whatever-Vant kubwa ili ujipongeze na kisha lipia mwenyewe halafu basi.
 
Yeah hii gari subaru,Altezza zote haziingizi mguu sema ndio hivyo una changanoto nyingi kumbe hasa muundo wa injino yake rotary engine..injini hizi kumbe kila baada ya 100k unatakiwa uibadilishe na pia fuel consumption nasikia ni kubwa kwa kweli 1 kilometer zinakatika lita 8 za petrol imagine.
1km kwa 8liters! Hilo ni gari au ni kifaru cha jeshi?

Maana yake ni kwamba 100km inaficha 800ltrs ama pipa4?

Haiwezekani na hakuna gari la hivyo na si Tz tu, halipo duniani.
 
Back
Top Bottom