NISSAN NOTE
Sasa nakuja na chombo ya mjapani NISSAN NOTE ... Hii nayo ni HATBACK ina viti 5 ... Hukubkwa ndani ikiwa na mpangilio mzuri wa viti na nafasi ya viti kati ya lkn pia upande wa nyuma inakuja na nafasi kubwa ya kuweza kuweka mizigo hebu tuone
Gari hiii inakuja na
Hatchback
Extras: Navigation, Reverse
Camera, USB Charging
Safety Features: ABS, Electronic
Stability Control, SRS Airbags
Exterior Features: Alloy Rims,
Fog Lights, Spoiler
Interior Features: A/C, Aux Power, CD/DVD Player
Nissan Note ilianza kuzalishwa mwaka 2005 na kuuzwa katika soko la Japan na kwenye masoko mengine
1. first generation ilijulikana kama E11 na ilianza kuzalishwa kutoka mwaka 2005 hadi 2013.
2 second generation ilijulikana kama E12 ambayo ilianza kuzalishwa mwaka 2012 hadi leo jina la sokoni ilijulikana kama Nissan Versa na washindanj wake Honda Fit, Toyota Ractis na Mazda Demio.
Upande wa injini
Inakuja Nissan Note is offered wanakuja na machaguo mawili 2 ya injini
1200cc HR12DDR supercharged engine
1200 cc HR12DE normally aspirated engine.
Transmition ni XTRONIC CVT transmission na inapatikana kwa chaguo la 2WD na 4WD.
Hapa ndio utajua kuna brand zaidi ya toyota zipo vizuri
Upande wa acceleration wa injini hizi ..hiki kipengele nimekirudisha baad ya kushauriwa na baadhi ya watu ila cha mafuta ndio nafikiria nikiondoe
nawatania tu
Supercharged 1.2L Nissan Note accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 11.8 sec.
Normally Aspirated 1.2L Nissan Note accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 13.8 sec.
Hebu tuangalie grade za gari hili ni shida
2012 Nissan Note Grades
Nissan Note S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DE engine, Key start, manual AC, Radio/CD player, na 14-Inch steel rims
Nissan Note X – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DE engine, smart start, manual AC, Radio/CD player na 14-Inch steel rims
Nissan Note X FOUR – Toleo hili linakuja 1.2L HR12DE engine, 4WD, smart start, manual AC, Navigation/Infotainment and 15-Inch alloy rims
Nissan Note S DIG-S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment na 14-Inch steel rims
Nissan Note X DIG-S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment and 14-Inch steel rims na fog lights.
Nissan Note MEDALIST – luxury grade linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment and 15-Inch alloy rims na fog lights.
Uzuri wa gari hili nachopendea
1.Muonekano mzuri wa umbo lake
2.nafasi kubwa kwa ndani
3.matumizi mazuri ya mafuta tulia utaona hata ucjali nakumbuka
4.bei ya kulinunua ni ndogo sana
5.service yake kwa mwez haizid sh 30,000/- gharama ni ndogo sana
6.linavumilia mazingira ya aina yoyote
Hebu tuangalie kipengele cha mafuta maana hapa ndio watu huwa wanakodolea macho
hapa ndio utajua mjapani alipindua meza kibabe sana lkn pia mjapani kachukua ugali kaumwagia maji ya kunawa
2012 Nissan Note inatumia km 25.2 Kwa lita 1
Hii ni kwa injini zote mbili zinatumia kiwango sawa cha mafuta
Haya hebu niambie hapo mjapani hajamjibj mjerumani kwa kumwagia ugali maji ya kunawa
Nisichokipenda katika gari hii
1.Kuja na injini mbili zenye cc sawa 1200 cc huku moja ikionekana inaufanisi mzuri wa kuhimili kuliko nyingine ...japo kiwango cha mafuta zipo sawa siitaji hiyo injini staki kuharibu biashara nifate bobo utoe shekeli nikushauli
2.muundo naona kama wameigana na honda fit
Kuhusu sapre
Zipo narudi zipo za kutosha hilo ondoa shaka kabisa
GROUND CLEARENCE
Hapa bwana gari hii inakuja na 6.1inch kwa umbo lake mm nasema iko sawa popote inaenda iwe mjini au kijijini
Kwenye ndoa
Hizi gari za nissani nyingi ndoa yake ni ngumu hii ni ndoa ya kikatoriki kwa wale wanaopenda kutoa taraka na kuoa tena au kuolewa hapa utapata shida kwenda kwa baba paroko
Mwisho kwa ushuri wangu
Naomba unisikilize kwa umakini kama wewe ni mtumishi au mjasiriamali hii gari inakufaaa açhana na wafanya biashara wanaonunua na kutumia ...wengine ni mabishoo wanapenda kuonekana na magari kila baada ya muda ...usiangalie maisha ya mwingine angalia ya kwako ....duniani hapa huwezi kumfurahisha kila mtu ,Mungu akusaidie macho yako yafunguke uone hazina iliyofichika karibu sana ulimwengu wa nisanin
Tuangalie na honda fit uweze kulinganisha mwenyewe wapi kuna unafuu
Najua kwa muda mrefu umewahi kuyasikia magari ya honda ....ni moja kati ya brand moja nzuri ambayo wamarekani wanaizimia sana na kuielewa vilivyo
Gari hili ni gari dogo zuri narudia tena zuri sana linamuonekano wa kishua sana huku likiwa na gharama ndogo sana
Moja kati ya gari ambazo haziuzwi hela kubwa sio kwa sababu hazina wateja hapana ...ila wanajitahidi kuwafikiwa watubwa kipato cha chini
Gari hilinlinakuja na machaguo mawili ya engine ingine ya kwanza ni cc 1300 na engine ya pili ni cc1500 huku likiwa na mfumo madhubuti kabisa katika silinder head na kulifanya kuyashinda magari ya toyota kwa utumiaji mzuri wa mafuta
Uwezo wa tank la gari hili linaa chukua lita 42 za petrol ....ni mojankati ya gari ambalonlipo katika kundi la magari madogo gari hili huwezi kulilinganisha na toyota IST WALA RAUMU ,AU VITS japo ni dogo
Gari hili linasifa za pekeee linakuja na siti za kukaaa watu 5 kama ilivyo familia nyingi huwa hazizidi watu watano ...hivyo kulifanya lifae kwa matumizi ya ya familia
Kwa ndani gari hili linakuja na redio ,usbbport ,na mfumobwa aple na android hivyo kutoa nafasinkwa mtumiaji kuuunganisha nankuweza kusikiliza nyimbo kupitia simu yake lakininpianlina vifaa vya halinya hewa hivyo kukuonyesha unakoenda halinikoje na kuchukua tahadhari
Hebu tuangalie grade za honda fit
2013 Honda Fit Grades
Honda Fit 13G: hii inakuja na chaguo la 1300cc engine na inakuwa na features kama Air Conditioner, Automatic Transmission, ABS, 13inch Steel rims or 14 Inch Alloy Rims, CD/Navigation system, Driver and Passenger Airbags, and Fog Lights on some.
Honda Fit 15G: Toleo hili linakuja na 1500cc na Air Conditioner, Automatic Transmission, ABS, 13inch Steel rims or 14 Inch Alloys, CD/Navigation system, Driver and Passenger Airbags, Fog Lights on package editions
Honda Fit RS: hili nintoleo maalumu kwa ajili ya michezo ya magari linakuja na injini yenye nguvu sana t suspension that features heavy duty coilovers, front and rear disc brakes and 16 Inch Alloy rims. It comes with the 1500cc engine that has been tuned for extra power and mated to a 6 Speed Manual Transmission or a 5 speed Auto. On the exterior, it has a body kit, fog lights na rear spoiler.
Hebu angalia uwezo wa gari hili lilivyo wa ajabu katika utumiajinwa mafuta ambao unakusaidia kutumia pesa kidogo na huku likikufanyabuwe na trip nyingi kwa town
Tuangalie utumiaji wake wa mafiuta hapa ndipo utaipenda honda
Honda Fit Fuel Consumption
Honda Fit 13G inatumia km 20.6 kwa lita 1
Honda Fit 15G inatumka km19.0 kwa lita 1
Honda Fit RS inatumia km 16.2 kwa lita 1
Honda Fit Acceleration
Honda Fit 13G accelerates kutoka 0-100 km/h kwa12.1 secs.
2013 Honda Fit 15G accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 10.9 secs.
Honda Fit RS accelerates kutoka 0-100 km/hkwa 9.6 secs
Jamani hebu changamkieni gari hili linakuja na mfumo wa ABS ,na sensor ambazo zinasaidia kuonyesha matumizi ya vifaa anwai kwenye gari hili
Uzuri wa gari hili
*Matumizi madogo sana ya mafuta
*Linahitaji service chache tu
*Linausalama mzuri kwa mtumiaji
*Gari hili lina teknolojia rahic fundi yoyote ananuwezo wa kulitengeneza hata mafundi spana na nyundo
*Linafaa kwa matumizi ya uber
Changamoto
*Vipuli vyake ni adimu ila vipo vinapatikana baadhi bei rahic vingine ndio pesa kubwa
*Linachelewa kuchanganya speeed ...kwa baadhi ya grade ila kwa toleo la cc 1500 ni moto
rx8,alltez ,subaru wanasumbuana barabarani hukunikiwafata kwa nyuma
GROUND CLEARENCE YA GARI HILI
upande wa uvungu wa gari sio haba lipo juu kwa umbo lake na gravity ni sawa ina 5.9 inch iko poa hata vijijini unaenda nayo ila kama unataka kuitumia kama uber au tax nakushauri uinue kidogo tu isogee kwenye 6.5 inch
Unalipataje gari hili ukiamua kuliagiza mpka linafika mikonon mwako litakugharimu kiasi cha sh 8 milion mchanganuo upo hivi kama utaagiza
Bei ya gari huko japan ni dlollar 1390
Bank change. Dollar 60
Total CIF. Dollar1450
Ushuru. TRA 3,882,566
BANDARI. sh 640,000
Agent 200,000
Jumla ya hela yote ni sh 8MILION