Naomba kujuzwa matatizo ya Nissan Note na Honda Fit

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,680
1,500
Wadau habari,

kwa wale wataalaamu wa magari nnaomba msaada wenu kujua haya magari tajwa hapo juu ukiachilia mbali swala la ulaji wa mafuta, yana matatizo gani na je Kama nikitaka kununua moja kati ya gari hizo utashauri ninunue gari gani?

Binafsi nnazipenda saana hizo gari, na Mwezi ujao nnataraji kuagiza moja kati ya hizo.

Asanteni

1591786315993.png

Nissan Note

1591786391744.png

Honda Fit
 

chicotton

Member
Feb 14, 2013
37
0
Nakushauri uangalie zaidi nissan note yenyewe ni imara spare zake zinadum sana japo upatikanaji wake sio kama wa toyota. Iyo honda hamna kitu hapo
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,935
2,000
Nakushauri nissan,ukiweza angalia sbtjapan.com huenda zipo zilizofika Dar tayari.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
30,847
2,000
Nakushauri uangalie zaidi nissan note yenyewe ni imara spare zake zinadum sana japo upatikanaji wake sio kama wa toyota. Iyo honda hamna kitu hapo
ila Honda ni gari ambayo inakubalika sana marekani kwa reliability ikifuatiwa na Toyota.
 

bizplan

JF-Expert Member
Jun 28, 2013
466
500
Wadau habari,
kwa wale wataalaamu wa magari nnaomba msaada wenu kujua haya magari tajwa hapo juu ukiachilia mbali swala la ulaji wa mafuta, yana matatizo gani na je Kama nikitaka kununua moja kati ya gari hizo utashauri ninunue gari gani?
Binafsi nnazipenda saana hizo gari, na Mwezi ujao nnataraji kuagiza moja kati ya hizo.
aksanteni View attachment 127355 View attachment 127356

Kwanza lazima ni-admit honda fit mbali na kuiona ktk picha sijawahi imiliki. Kuhusu note nimeshakuwa nazo mbili sasa. Tofauti tu ni kuwa wewe umeweka model za 2005 hadi 2007 katika hiyo picha. Wakati kwa upande wangu nitumetumia model za 2008 hadi 2012. By the way tofauti ya hizo model mbili ni ndogo sana hasa show grill.

Nije kwenye swali lako, ubaya wa note ni upi? Kwa upande wangu note imekuwa na changamoto Kutokana na urefu wake na vile tumbo lake lipo chini so unaweza kuwa na tatizo la kugonga chini hasa kwenye mashimo. Kutatua tatizo hili hakikisha unainyanyua juu, badili rim size toka 13 hadi 14 au 15 na tairi 185 au 195 utakuwa umepunguza tatizo.

Kuhusu uimara, hii gari ni imara sana sana yaani inazizidi gari nyingi za aina yake. Imagine mvua za Dar zimenyesha tangu August/September madimbwi kila kona lakini gari ipo vzr. Spea zake zinadumu muda mrefu sana. Hizi gari zinakimbia sana, kutoka 0-100 ni muda mfupi sana. Pia ni nzito na stable barabarani. Kwa kweli ni gari nzuri sana. Watu wengi ambao wameona nimekuwa nazo nyingi wameanza kuzipenda sana. Nitoe mfano: IST ambazo zinapendwa na wengi, kwa Note hazitii mguu kabisaaa sio kwa spidi, stability, uimara yaani imezidiwa karibu vitu vyote.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,613
2,000
Kwanza lazima ni-admit honda fit mbali na kuiona ktk picha sijawahi imiliki. Kuhusu note nimeshakuwa nazo mbili sasa. Tofauti tu ni kuwa wewe umeweka model za 2005 hadi 2007 katika hiyo picha. Wakati kwa upande wangu nitumetumia model za 2008 hadi 2012. By the way tofauti ya hizo model mbili ni ndogo sana hasa show grill...
Hahah bila shaka hio note yako ni 1.5 L HR15DE ambayo inatoa 109HP na Ki-Ist cha 1.5 1NZ-FE kinatoa 109hp hio hio nyie wote hamchekani aisee, halafu hivi vibebi walker kuvipigia mbwembwe za 0-100 katakuja kukubastia tu mjomba haviku tengenezwa kupigia vurugu hizo mkuu.
 

Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,741
2,000
Hahah bila shaka hio note yako ni 1.5 L HR15DE ambayo inatoa 109HP na Ki-Ist cha 1.5 1NZ-FE kinatoa 109hp hio hio nyie wote hamchekani aisee,halafu hivi vibebi walker kuvipigia mbwembwe za 0-100 katakuja kukubastia tu mjomba haviku tengenezwa kupigia vurugu hizo mkuu.
Mkereketwa wa Nissan nimekuja...

Hivi vibaby Walker, wallah Note ni tamu...
Nimeendesha Ist,Vitz na Swift....ni gari nzuri ila hazipo comfortable kama hii Nissan note....nadhan Wheel base ya Nissan ni kubwa kuliko hizo IST..IST ni fupi kwa hiyo kanakuwa kama kanadunda dunda hivi..

Huu ni uzoefu binafsi...
Mnaruhusiwa kunikosoa..
 

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
999
2,000
NISSAN NOTESasa nakuja na chombo ya mjapani NISSAN NOTE ... Hii nayo ni HATBACK ina viti 5 ... Hukubkwa ndani ikiwa na mpangilio mzuri wa viti na nafasi ya viti kati ya lkn pia upande wa nyuma inakuja na nafasi kubwa ya kuweza kuweka mizigo hebu tuone

Gari hiii inakuja na

Hatchback
Extras: Navigation, Reverse
Camera, USB Charging
Safety Features: ABS, Electronic Stability Control, SRS Airbags
Exterior Features: Alloy Rims, Fog Lights, Spoiler
Interior Features: A/C, Aux Power, CD/DVD Player

Nissan Note ilianza kuzalishwa mwaka 2005 na kuuzwa katika soko la Japan na kwenye masoko mengine
1. first generation ilijulikana kama E11 na ilianza kuzalishwa kutoka mwaka 2005 hadi 2013.
2 second generation ilijulikana kama E12 ambayo ilianza kuzalishwa mwaka 2012 hadi leo jina la sokoni ilijulikana kama Nissan Versa na washindanj wake Honda Fit, Toyota Ractis na Mazda Demio.

Upande wa injini
Inakuja Nissan Note is offered wanakuja na machaguo mawili 2 ya injini

1200cc HR12DDR supercharged engine

1200 cc HR12DE normally aspirated engine.

Transmition ni XTRONIC CVT transmission na inapatikana kwa chaguo la 2WD na 4WD.

Hapa ndio utajua kuna brand zaidi ya toyota zipo vizuri

Upande wa acceleration wa injini hizi ..hiki kipengele nimekirudisha baad ya kushauriwa na baadhi ya watu ila cha mafuta ndio nafikiria nikiondoe nawatania tu

Supercharged 1.2L Nissan Note accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 11.8 sec.

Normally Aspirated 1.2L Nissan Note accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 13.8 sec.

Hebu tuangalie grade za gari hili ni shida

2012 Nissan Note Grades

Nissan Note S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DE engine, Key start, manual AC, Radio/CD player, na 14-Inch steel rims

Nissan Note X – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DE engine, smart start, manual AC, Radio/CD player na 14-Inch steel rims

Nissan Note X FOUR – Toleo hili linakuja 1.2L HR12DE engine, 4WD, smart start, manual AC, Navigation/Infotainment and 15-Inch alloy rims

Nissan Note S DIG-S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment na 14-Inch steel rims

Nissan Note X DIG-S – Toleo hili linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment and 14-Inch steel rims na fog lights.

Nissan Note MEDALIST – luxury grade linakuja na 1.2L HR12DDR supercharged engine, smart start, automatic AC, Navigation/Infotainment and 15-Inch alloy rims na fog lights.

Uzuri wa gari hili nachopendea

1.Muonekano mzuri wa umbo lake

2.nafasi kubwa kwa ndani

3.matumizi mazuri ya mafuta tulia utaona hata ucjali nakumbuka

4.bei ya kulinunua ni ndogo sana

5.service yake kwa mwez haizid sh 30,000/- gharama ni ndogo sana

6.linavumilia mazingira ya aina yoyote

Hebu tuangalie kipengele cha mafuta maana hapa ndio watu huwa wanakodolea macho hapa ndio utajua mjapani alipindua meza kibabe sana lkn pia mjapani kachukua ugali kaumwagia maji ya kunawa

2012 Nissan Note inatumia km 25.2 Kwa lita 1

Hii ni kwa injini zote mbili zinatumia kiwango sawa cha mafuta

Haya hebu niambie hapo mjapani hajamjibj mjerumani kwa kumwagia ugali maji ya kunawa

Nisichokipenda katika gari hii

1.Kuja na injini mbili zenye cc sawa 1200 cc huku moja ikionekana inaufanisi mzuri wa kuhimili kuliko nyingine ...japo kiwango cha mafuta zipo sawa siitaji hiyo injini staki kuharibu biashara nifate bobo utoe shekeli nikushauli

2.muundo naona kama wameigana na honda fit

Kuhusu sapre
Zipo narudi zipo za kutosha hilo ondoa shaka kabisa

GROUND CLEARENCE
Hapa bwana gari hii inakuja na 6.1inch kwa umbo lake mm nasema iko sawa popote inaenda iwe mjini au kijijini

Kwenye ndoa

Hizi gari za nissani nyingi ndoa yake ni ngumu hii ni ndoa ya kikatoriki kwa wale wanaopenda kutoa taraka na kuoa tena au kuolewa hapa utapata shida kwenda kwa baba paroko

Mwisho kwa ushuri wangu
Naomba unisikilize kwa umakini kama wewe ni mtumishi au mjasiriamali hii gari inakufaaa açhana na wafanya biashara wanaonunua na kutumia ...wengine ni mabishoo wanapenda kuonekana na magari kila baada ya muda ...usiangalie maisha ya mwingine angalia ya kwako ....duniani hapa huwezi kumfurahisha kila mtu ,Mungu akusaidie macho yako yafunguke uone hazina iliyofichika karibu sana ulimwengu wa nisanin
Tuangalie na honda fit uweze kulinganisha mwenyewe wapi kuna unafuuNajua kwa muda mrefu umewahi kuyasikia magari ya honda ....ni moja kati ya brand moja nzuri ambayo wamarekani wanaizimia sana na kuielewa vilivyo
Gari hili ni gari dogo zuri narudia tena zuri sana linamuonekano wa kishua sana huku likiwa na gharama ndogo sana

Moja kati ya gari ambazo haziuzwi hela kubwa sio kwa sababu hazina wateja hapana ...ila wanajitahidi kuwafikiwa watubwa kipato cha chini

Gari hilinlinakuja na machaguo mawili ya engine ingine ya kwanza ni cc 1300 na engine ya pili ni cc1500 huku likiwa na mfumo madhubuti kabisa katika silinder head na kulifanya kuyashinda magari ya toyota kwa utumiaji mzuri wa mafuta

Uwezo wa tank la gari hili linaa chukua lita 42 za petrol ....ni mojankati ya gari ambalonlipo katika kundi la magari madogo gari hili huwezi kulilinganisha na toyota IST WALA RAUMU ,AU VITS japo ni dogo

Gari hili linasifa za pekeee linakuja na siti za kukaaa watu 5 kama ilivyo familia nyingi huwa hazizidi watu watano ...hivyo kulifanya lifae kwa matumizi ya ya familia

Kwa ndani gari hili linakuja na redio ,usbbport ,na mfumobwa aple na android hivyo kutoa nafasinkwa mtumiaji kuuunganisha nankuweza kusikiliza nyimbo kupitia simu yake lakininpianlina vifaa vya halinya hewa hivyo kukuonyesha unakoenda halinikoje na kuchukua tahadhari

Hebu tuangalie grade za honda fit
2013 Honda Fit Grades

Honda Fit 13G: hii inakuja na chaguo la 1300cc engine na inakuwa na features kama Air Conditioner, Automatic Transmission, ABS, 13inch Steel rims or 14 Inch Alloy Rims, CD/Navigation system, Driver and Passenger Airbags, and Fog Lights on some.

Honda Fit 15G: Toleo hili linakuja na 1500cc na Air Conditioner, Automatic Transmission, ABS, 13inch Steel rims or 14 Inch Alloys, CD/Navigation system, Driver and Passenger Airbags, Fog Lights on package editions

Honda Fit RS: hili nintoleo maalumu kwa ajili ya michezo ya magari linakuja na injini yenye nguvu sana t suspension that features heavy duty coilovers, front and rear disc brakes and 16 Inch Alloy rims. It comes with the 1500cc engine that has been tuned for extra power and mated to a 6 Speed Manual Transmission or a 5 speed Auto. On the exterior, it has a body kit, fog lights na rear spoiler.

Hebu angalia uwezo wa gari hili lilivyo wa ajabu katika utumiajinwa mafuta ambao unakusaidia kutumia pesa kidogo na huku likikufanyabuwe na trip nyingi kwa town

Tuangalie utumiaji wake wa mafiuta hapa ndipo utaipenda honda

Honda Fit Fuel Consumption

Honda Fit 13G inatumia km 20.6 kwa lita 1

Honda Fit 15G inatumka km19.0 kwa lita 1

Honda Fit RS inatumia km 16.2 kwa lita 1

Honda Fit Acceleration

Honda Fit 13G accelerates kutoka 0-100 km/h kwa12.1 secs.

2013 Honda Fit 15G accelerates kutoka 0-100 km/h kwa 10.9 secs.

Honda Fit RS accelerates kutoka 0-100 km/hkwa 9.6 secs

Jamani hebu changamkieni gari hili linakuja na mfumo wa ABS ,na sensor ambazo zinasaidia kuonyesha matumizi ya vifaa anwai kwenye gari hili

Uzuri wa gari hili
*Matumizi madogo sana ya mafuta
*Linahitaji service chache tu
*Linausalama mzuri kwa mtumiaji
*Gari hili lina teknolojia rahic fundi yoyote ananuwezo wa kulitengeneza hata mafundi spana na nyundo
*Linafaa kwa matumizi ya uber

Changamoto
*Vipuli vyake ni adimu ila vipo vinapatikana baadhi bei rahic vingine ndio pesa kubwa

*Linachelewa kuchanganya speeed ...kwa baadhi ya grade ila kwa toleo la cc 1500 ni moto rx8,alltez ,subaru wanasumbuana barabarani hukunikiwafata kwa nyuma

GROUND CLEARENCE YA GARI HILI
upande wa uvungu wa gari sio haba lipo juu kwa umbo lake na gravity ni sawa ina 5.9 inch iko poa hata vijijini unaenda nayo ila kama unataka kuitumia kama uber au tax nakushauri uinue kidogo tu isogee kwenye 6.5 inch

Unalipataje gari hili ukiamua kuliagiza mpka linafika mikonon mwako litakugharimu kiasi cha sh 8 milion mchanganuo upo hivi kama utaagiza

Bei ya gari huko japan ni dlollar 1390
Bank change. Dollar 60
Total CIF. Dollar1450
Ushuru. TRA 3,882,566
BANDARI. sh 640,000
Agent 200,000
Jumla ya hela yote ni sh 8MILION
 

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
3,960
2,000
Hakuna Nissan Note ya 1.2 L na hakuna nissan notr yenye conspt ya mafuta 25.1 km/L, na hiyo gari sio daraja moja na ist bali ni raum na jamii za gari ya toyota zenye cc1490/cc1500
 

Mlolongo

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
935
1,000
Hahah bila shaka hio note yako ni 1.5 L HR15DE ambayo inatoa 109HP na Ki-Ist cha 1.5 1NZ-FE kinatoa 109hp hio hio nyie wote hamchekani aisee,halafu hivi vibebi walker kuvipigia mbwembwe za 0-100 katakuja kukubastia tu mjomba haviku tengenezwa kupigia vurugu hizo mkuu.

Habari. Unamjua rafiki yako mwenye Honda Fit nzuri au VITZ? Natafuta sana sipati
 

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,831
2,000
Nakushauri uangalie zaidi nissan note yenyewe ni imara spare zake zinadum sana japo upatikanaji wake sio kama wa toyota. Iyo honda hamna kitu hapo
Unaijua vizuri hiyo honda lakini? au ndio zile story za vijiweni?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom