Naomba kujua maeneo ya kucheki movies kwa hapa Mwanza

Salaam wakuu
Mie ni mgeni kwa hapa Mwanza napenda kujua maeneo ya kucheki movies kama vile mlimani city na Quality centre kwa Dar es salaam.
Rock city mall kuna ukumbi wa sinema ila sidhani kama wameshaanza kuonesha
 
Salaam wakuu
Mie ni mgeni kwa hapa Mwanza napenda kujua maeneo ya kucheki movies kama vile mlimani city na Quality centre kwa Dar es salaam.
Ngosha hawana muda wa kuangalia movie wala nini wao ni kazi tu mkuu..hope umetokea Dar mkuu??
 
Panda gari za Igombe, mwambie konda akushushe kwa Maliganya, hapo kuna movie kali, kitu 3D unapewa miwani yako kabisa!
 
Haya mambo si kila mahali ni ya kawaida, movie theaters Mwanza zilikuwepo zamani, mapinduzi ya teknolojia yakaharibu soko lake baada ya mzee wa ruksa kushika madaraka, kwa sasa nadhani priorities Mwanza ni maendeleo ya miundombinu na mengineyo, hakuna mwekezaji anawaza kuwekeza mamilioni ya pesa kujenga movie theater wakati kila mtu nyumbani anamiliki flat screed ya 3D na mengineyo mengi. Vuta subira labda CINEMAX watakuja Mwanza, kwa sasa nenda pale mjini kati kajitwalie flat screen yako ukute unajipunguzia machungu!
 
Back
Top Bottom