Naomba kujua kuhusu mabalo ya mtumba ya nguo za watoto

Nunua chapa za kanada. Kuna kampuni inaitwa giga. Kama vipi nikupeleke mnazi mmoja lete ofa yako twende kesho
 
Ok.
Primary hint.
Mitumba ni bidhaa zilizowahi kutumika zinazouza mara ya pili (second hand). Mitumba ni broad sense ya bidhaa tofauti tofauti ikiwemo nguo, magari.. mashine mbalimbali nk. Somo la Leo litaelezea mitumba ya nguo.

Biashara ya mitumba ilianza rasmi miaka ya 1986, kipindi cha mkataba wa ruksa. Ulioruhusu excess importation. Mitumba hutoka nchi za Dunia ya kwanza kwenda ya pili au ya tatu.

Tz inapokea mitumba kutoka China, UK, Australia, Korea, Canada na nchi za Arabs hasa Dubai, Pakistan.
 
Mitumba ya hutofautiana ubora. Kifaa kikitumika hakiwezi kuwa Bora kama kipya. Bidhaa hiyo inakuwa na hali iliyichangiwa na aina ya matumizi, mfano ilitumika gereji.

Aina ya mtumiaji au muda iliyotumika
Mtumiaji huathiri hali ya kitu kwani watu wengine hawajali vitu, hivyo vitu hivi huchoka au kuchakaa sana, mapema mnoo.
Pia kitu kilichotumika muda mrefu huchoka zaidi.
 
Mitumba ya nguo hufungwa kwenye furushi moja lenye uzito maalum. Pia Huwa na cluster!. Yani huwekwa kulingana na ubora. Kwa namna hiyo mitumba hutokea katika vifurushi vyenye makundi ya gredi.. Yani gredi A, gredi B, gredi C. Yani Kuna mitumba michafu sana Yani LONYA na mitumba yenye ahueni
 
Sir Midabwada vipi kuhusu mabalo ya viatu, msaada tafadhali.
Shida ya biashara ya viatu inawafelishaga watu sehem moja.
Kuna tofauti kubwa kati ya viatu vizuri na viatu unavyovipenda. Ukinunua belo aidha la viatu au nguo kuna bidhaa mule hazitakivutia tu.. hizi utauza Bei chee hapo ndo pa kuwa napo makini
 
nunua chapa za canada, hapa kasulu ni bei rahisi kuliko dar es salaam maana zinatokea hapo Congo.
Kasulu ipi? Kasulu hapo hakuna mitumba hata grade C hupati, huko ni zile grade ya mwisho ya sh 1000/

Kwansaza watu wa huko hawavai mitumba wanapenda specila na soecila zenyewe ni zile rahisi rahisi, kitendo cha wao kuto pendelea mitumba kinafanya hata wauza mitumba wasilete nguo za maana.

Nimekaa huko nafanya kazi mashirka ya Umoja wa Mataifa,nguo za mitumba ilikuwa inabidi tungoje safari za Dar au Arusha, na Moshi ndio tukanunue, angalua kiasi Kahama.

Sio tu Kasulu, hio Kigoma nzima hakuna anaye leta Bellon Grade A wala B hata C


acha kudanganya watu humu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…