Nimekuwa nikijiuliza sana, pamoja na ufisadi mkubwa uliofanywa na kikwete na CCM kwa ujumla ambao hakuna mtanzania yeyote anayeweza kupinga ,maana kila kitu kiko wazi na hata CCM wanakili kufanya ufisadi huo!!. Kwa nini basi bado kuna watanzania wanamshabikia kikwete??, Tena nasikia huko kusini wamehaidi kumpa kura nyingi tu!!
Naomba nieleweshwe mambo yafuatayo
Je, wananchi hawataki kuamini ufisadi uliofanywa na viongozi wao , ambao viongozi wao wamekiri kufanya ufisadi huo?
Je, ni ile dhana ya kusema kwamba wananchi walipo kuwa wanasema ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM, ni sawa na kuweka agano na miungu ya CCM? kwamba chochote watakachosema viongozi wa CCM kiwe kibaya ,kizuri fikra zao zidumu ni kweli?
Je, ni kwamba watanzania, hawajali maisha yao , ya watoto wao, ya wajukuu wao? ndo maana hawaoni umuhimu wa kuchagua viongozi wazuri na wenye nia njema na nchi yao?
Tope linaoza?Hii ndio BONGO au UDONGO?, wala sio UDONGO ni tope ilioza !! .
Elimu ya kutambulika ni elimu gani?,unafahamu elimu ya makamba? Kikwete atapambana vipi wakati yeye alifanya ufisadi. Pia elimu si kigezo, raisi Zuma hakwenda shule lakini ni kiongozi mzuri, Uongozi ni talents, si kusoma. Pia kaa uelewe chini ya uongozi wa CCM ufisadi hautapunguzwa. 'top layer' yote inanuka kwa rushwa, nani atamuwajibisha mwenzake? Usijidanganye.Wamekosa chama Mbadala, bora waendelee na CCM ambayo Kikwete ameahidi kupambana na ufisadi, kwani historia inaonyesha kuwa CCM wanajirekebisha mwaka hadi mwaka, chini ya uongozi wa Kikwete nchi inaweza fika mbali
Chadema hakiwezi kuwa chama mbadala kwa sababu ni chama kinaendeshwa kwa udini na ukabila na viongozi wake wote hawana elimu inayo tambulika, mfano:
M/Kiti Mbowe O Level
Mgombea Mweza drasa la saba
Mchungaji Slaaa kasomea bibilia
Kweli hawa ni watu wa kuwakabidhi nchi ? you must be kidding!!!