Naomba kuelekezwa jinsi ya ku-apply vyuo vya afya kupitia NACTE

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)



looogo.png



TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:
  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.

  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.

  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji
  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.


  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.


  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.


  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.


  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.

Angalizo: Kwa eneo la Mafunzo ya Ualimu na kozi ya Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (Community Health Workers) hayatakuwepo kwenye udahili wa awamu hii.

Bofya hapa kufanya maombi

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA VYUO

Imetolewa na:

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

23 Januari, 2017
 
Write your reply...santeee kk .. ila naomba kuuliza kitu kk mm nina phzx_C , bios_C na chem D (math C na english C) vp nina sifa ya kuchaguliwa vyuo vikuu kama muhas, lugalo n.k kama ni apply kwa vyuo hivyo kk..?
 
Kwa ufaulu huo utachaguliwa,kwa diploma level ,fani yoyote ya afya subiri tu udahili ufunguliwe
 
Back
Top Bottom