Bolingo Ya Telephone
Senior Member
- Jun 29, 2020
- 114
- 119
Wakuu,
Kweli nimeamini kuishi hapa Duniani ni gharama sana inatubidi tupambane haswa ndipo mambo yasituendee kombo. Kwanza kabisa mimi bado ni kijana mdogo tu umri wangu ni kati ya 26 na 28, nimeamua kuchukua hatua hii baada ya kuona mambo hayaendi sawa kabisa.
Kwasasa nafanya kazi/sijui niite ni kibarua kwenye kampuni flani binafsi kwa mkataba ila malipo yake ni madogo sana kiasi kwamba unajikuta unapata hela ya kula tu tena kwa kuunga unga, usipopiga bajeti kali kama chenga za Pele basi utajikuta hoi kabisa.
Malipo yake ili utoboe mwezi itakubidi ujibane haswa halafu mbaya zaidi Kampuni ina masharti makali haswa huwezi kupata hata nafasi ya kusema uende ukatafute hata kibarua ya aina yoyote ufanye kwa ajili ya kujiongezea kipato cha kujikimu. Kila siku ni wewe na kazi kazi na wewe na bado huko nyumbani wanakutegemea kwakweli ni inakua vigumu mno kwa kijana kuweka akiba hata kidogo kwa ajili ya maisha yake ya baadaye tena kwa sisi vijana wa kiume kulingana na taratibu na tamaduni zetu inafika wakati itakubidi utafute mwenza kwa ajili ya kuanzisha na kujenga familia sasa kwa hali kama hii inakua ni taabu kweli kweli.
Naomba kama kuna mtu ana mpango wa kulima kilimo biashara na anahitaji mtu wa kusimamia shamba hilo na kuhakikisha shamba linakua salama basi niko tayari tuwasiliane tufanye kazi pamoja kwa makubaliano, tunaingia mkataba na ningependa kwenye mkataba wetu iwe kama ifuatavyo:-
1) Ukubali kuwa mwenyeji wangu huko
2) Unitafutie na unihakikishie mahali pa kujistiri; ukipata ka single room kadogo kabisa itapendeza zaidi ila hapa utakua unalipia kodi ya hako kageto
3) Ukubali kunilipa robo ya mapato yote yatakayopatikana kwenye mauzo ya mazao yote shambani, kwani nitakua shambani kama kibarua na wakati huo huo pia nipo kama msimamizi/muangalizi wa shamba
4) Mazao yawe ni ya muda mfupi isiyozidi miezi minne
5) Kwenye msosi nitajisimamia mwenyewe (ila ukipenda pia unaweza kunipiga tafu siku moja moja- hii ni nje ya mkataba)
Wakuu, mpaka nimeamua kuchukua hatua kama hii ya kuleta bandiko humu ni kuwa niko serious kweli kweli na haya maisha, nitafanya kazi kwa kufuata maelekezo yako.
Nitafanya kazi kwa bidii haswa ili tuweze kufanikiwa kwa pamoja kwani najua endapo nitazembea na kusababisha kufeli katika hazima yetu hiyo basi tutaumia sote haswa wewe na hata mimi kwakuwa nitakua nimechoma miezi yangu minne bila lengo kusudiwa kutimia hakika sitokubali kitu kama hicho kitokee!
Wakuu, kwa utii na unyenyekevu wa hali ya juu kwenu, naomba kama kuna aliyeguswa na bandiko hili na ana mpango kama huu basi anitafute PM ili tubadilishane mawasiliano kusudi tuweze kuwasiliana tuongee kwa mapana zaidi, ningependa tuanze msimu wa mwezi wa kumi/kilimo cha kumuagilia au hata ya kutegemea rehema za Mwenyezi Mungu pia siyo mbaya. Ahsante sana!
Kwa vijana wenzangu, najua mimi ni mmoja tu kati ya vijana maelfu kwenye Jamhuri yetu hii tukufu ya Tanzania ambao tunapitia hali kama hii ila tusife moyo/tusikate tamaa chamsingi tuendelee kuchapa kazi na tuwe waaminifu. Mtu akikupa kazi yake kuwa muaminifu kwani tabia njema ni silaha.
Tupambane haswa kwa imani iko siku kwa imani nasi tutafanikiwa tu!