Nani zaidi kati ya Hamie Rajab, Eddie Ganzel, Elvis Musiba, Ben Mtobwa?

Dibo10

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,307
1,583
Kama kuna kitu kinakosekana katika taasisi zote za kiswahili ni kushindwa kuwaenzi waandishi mahiri kabisa waliotikisa viunga vya Afrika Mashariki kwa masimulizi yenye kuchetua nyoyo za wasomaji.

Hebu tukumbushane ni nani zaidi kwako, kati ya waandishi uliowahi kusoma vitabu vyao, ambao masimulizi yao yameacha athari ktk kumbukumbu zako.

Je, ni Shabani Robert? Marehem Bawji? JoHn Kaduma? Taja mwandishi yoyote na na kitabu chake au hadith yake, maana kuna baadhi ya waandishi walikuwa wanatoa hadithi zao ktk magazeti.
 
Shaban Robert, Said Said (Kiu), Msiba na vitabu vyake vya ukombozi, tusisahau vitabu tulivyosoma vya Alan Quaterman na alflera ulela sababu ingawa watunzi si waswahili lakini vilifasiriwa na vikatupa uhondo.
 
Shaban Robert, Said Said (Kiu), Msiba na vitabu vyake vya ukombozi, tusisahau vitabu tulivyosoma vya Alan Quaterman na alflera ulela sababu ingawa watunzi si waswahili lakini vilifasiriwa na vikatupa uhondo.
kizazi kile kilikuwa ni Golden era kwa waandishi wa kitanzania
 
Nilikuwa msomaji mzuri wa riwaya.

1. Hammie Rajab nilisoma riwaya yake ya "Roho Mkononi". Nyota katika kitabu kile alikuwa jasusi aliyeitwa Ray Sibanda. Ni riwaya nzuri mpaka leo naikumbuka. Nilikisoma zaidi ya mara nne.

2. Elvis Musiba na mfulululizo wa riwaya zake za jasusi zikimhusisha mpelelezi machachari Willy Gamba sitazisahau pia. Zimo "Njama", "Kikomo", "Hujuma" na kadha wa kadha.

Ni kwa nini utunzi na usomaji wa riwaya umefifia?
 
Back
Top Bottom