Derspiegel
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 285
- 242
Wakati wa michakato ha teuzi za wagombea urais, John Pombe Magufuli alikuwa mmoja kama siyo aliyeongoza kwa kutamaniwa na makundi tofauti nchini, isipokuwa kwamba haikutarajiwa kuwa atapita mbele ya wababe wa Chama hasa Lowassa na Membe.
Hata hivyo baada ya kuvuka viunzi vya Baraza la Wazee, CC, NEC na mkutano mkuu, alionekana pia kukubalika kwa wananchi wasio na milengo ya vyama. Hata hivyo hakuna aliyetqrajia kuwa huyu Mgombea wa CCM angeweza kuleta mabadiliko makubwa nchini hasa katika kubana matumizi yasiyo ua lazima kwa kupunguza safari nje, kufuta baadhi ya sherehe, posho na semina kwa idara na ofisi za Serikali. Hali hii ilipelekea mgongano wa kimaslahi kwa waliofaidika na mifumo hiyo.
Hata hivyo, ukiachana na mengine mengi yaliyohusu utumbuaji wa majipu, kitendo cha Rais kubana mianya ya wakwepa kodi ndilo chimbukp kubwa la matatizo yanayoendelea sasa nchini kiasi cha baadhi ya watu wenye fikfa ndogo wanamlaumu Rais.
Hivi ni kweli ndio sisi ''WADANGANYIKA'' tuliokuwa tunalilia mabadiliko ama wengine? Je mnadhani maghorofa yanayojengwa Dar es salaam na kuufanya kuwa mojawapo ya majiji yanayokuwa kwa kasi Afrika fedha zinatoka wapi? Nani anajua status ya wakulima wetu kwa sasa? Jaribuni kuelewa kuwa, nchi haitaendelea kamwe kwa kudekeza wafanyabiashara ambao wanatoa huduma na kuacha wazalishaji wasio na msaada.
Tumuunge Rais wetu kwani walioumia ni wengi mno wakiwemo wanaccm ambao wanaisoma namba pia lakini hao walikuwa wakitegemea njia ya mkato.
Nawasilisha.