Nani mwenye uelewa na hii Issue ya Bima Vikundi vya Mazishi ya NMB

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Kwa niaba ya Benki ya NMB
Tunapenda kukujuza ndugu mteja/mwanafamilia ambaye upo kwenye kikundi chenye lengo la kusaidiana katika majanga kama kifo, tumekuja na Bima maalum iitwayo ( Group funeral Cover) yenye lengo la kusaidia vikundi na wanakikundi hasa katika janga la kifo..!Kweli NMB Karibu Yako!

lko hivi!!
Kikundi cha watu 15+ na umri wa miaka 18-70 wanaweza kukata bima ili kufidiwa pale janga la kifo linapotokea.
Bima hii iko katika vifurushi 3
1. BRONZE
Kila mwanakikundi atachangia TSh. 500 X 12 miezi; Na fidia itatolewa
  • Mwanakikundi -1,000,000/=
  • Mke/Mme - 1,000,000/=
  • Watoto hadi 4 - 500,000/=
2. SILVER
Kila mwanakikundi atachangia TSh. 1,200 X 12 miezi; Na fidia itatolewa
  • Mwanakikundi -3,000,000/=
  • Mke/Mme - 2,000,000/=
  • Watoto hadi 4 - 1,000,000/=
3. GOLD
Kila mwanakikundi atachangia Tsh.2,000 X 12 miezi; Na fidia itatolewa
  • Mwanakikundi -5,000,000/=
  • Mke/Mme - 4,000,000/=
  • Watoto hadi 4 - 1,000,000/=

Kwa maelezo zaidi,tembelea tawi lolote la Benki ya NMB lililopo karibu na wewe Majibu kamili kutoka kwa idara husika NMB:

Swali: Je kama mtu ana magroup zaidi ya moja anaruhusiwa kujiunga yote au kuchagua moja?

Jibu: Anaruhusiwa kujiunga kwenye kila group alilokuwepo mradi tu atalipia kwa kila group na pia atalipwa haki zake kupitia kila group alilokuwepo mpka kiwango cha juu kabisa cha Milion 15.

Swali: Je group linatakiwa kuleta document yoyote wakati wa kujiunga?

Jibu: Ndio na ni muhustari wa group unaoambatana na majina ya wanagroup wote. Ikionyesha namba zao za NIDA,auKadi ya mpiga kura, au leseni ya kuendesha gari, au hati ya kusafiria na kama wako nje ya nchi watahusika wale ambao ni watanzania tu na ambao wana NIDA, au kadi ya mpiga kura, au hati ya kusafiria au leseni ya kuendesha gari

Swali: Ni kwa nini hamkuweka wazazi?

Jibu: Wazazi wapo ila ni wa mchangiaji tu na si wakwe ila kwa bima ya gold mchango ni 8,500 kwa mwezi hivyo 102,000 kwa mwaka.Silver 5,500 kwa mwezi 60,000 kwa mwaka na Bronze 2,500 kwa mwezi na 30,000 kwa mwaka.

Swali: Je malipo yanafanyika kwa kila mwezi au kwa namna ipi?

Jibu: Wanagroup watalipa ada yao yote ya mwaka kwa mkupuo. Kwa gold ni 24,000 bila wazazi 102,000 wakiwepo wazazi.

Swali: Je mchangiaji ataanza kulipwa baada ya muda gani toka amejiunga na kutimiza taratibu zote?

Jibu: Hakuna kusuburi ni baada tu ya malipo kufanyika. Kuanzia hapo anakuwa na stahiki zote.

Swali: Je nani ataleta madai hapo benki na anakuja na nyaraka gani?

Jibu: Pesa italipwa kwa Admin wa group na yeye ndiye atampatia muhusika na au wale wote group itakaowapendekeza kwenye muhustasari wao.nyaraka zinazotakiwa wakati wa madai, Cheti cha kifo au kibali cha mazishi , na fomu ya madai.

Swali: Je kama group ni la familia na wamejiunga kifurushi chenye wazazi na watoto wapo 6 wanafiwa na Mzazi mmoja je malipo yanakuwaje?

Jibu: Kila mwanagroup atalipwa kwa kuwa alichanga.

NB: Familia haiwezi kuwa kikundi lakini familia moja inaruhusiwa wote kila mmoja kuwa mwanachama wa kikundi fulani.

Nimekuwa nikiona unatembea sana Kwenye Magroup ya WhatsApp.
 
Nionavyo Mimi, kampuni za Bima zina mitego mingi Sana. Pesa hazitolewi kirahisi namna hiyo. Wajanja Sana katika kutoa maelezo ambayo yanakuvutia. Subiri litakapokufika ndio uone sura yao ilivyo. Tatizo linapokufika utapenda ulipwe mafao yako mapema ili uweze kulitatua. Karaha unakuja pale unapoambiwa usubiri.
 
Daaaah umekuja na Hoja ya Msingi Sana na Wako Shallow kwenye maelezo Yao
 
Nionavyo Mimi, kampuni za Bima zina mitego mingi Sana. Pesa hazitolewi kirahisi namna hiyo. Wajanja Sana katika kutoa maelezo ambayo yanakuvutia. Subiri litakapokufika ndio uone sura yao ilivyo. Tatizo linapokufika utapenda ulipwe mafao yako mapema ili uweze kulitatua. Karaha unakuja pale unapoambiwa usubiri.

Sasa unataka ulipwe bila cheti cha kifo au kibali cha mazishi??
Hizi nyaraka ni muhimu sana. Pia hizi fedha ni za mkono wa pole na sio kuhudumia Msiba/ mazishi elewa hapo
 
Mimi shida yangu ipo wanaposema ..... Hata wana ndugu wa familia moja, kila mtu amekata bima kikundi kingine , hata kama mko wengi bado watamlipa kila mmoja hilo fao.

Hapo naona kuna mtego , cheti na kibali cha mazishi kitakuwa kimoja watalipaje kwa wote hao ?? Nani atakuwa na kibali? Ni dhahiri atakuwa mmoja na ndipo hapo kusaga meno kutakapo anza.. Tuwe makini na lengo la bima siku zote, sio mkata bima kupata faida ..
 
Hili linahitaji ufafanuzi.
 
Nionavyo Mimi, kampuni za Bima zina mitego mingi Sana. Pesa hazitolewi kirahisi namna hiyo. Wajanja Sana katika kutoa maelezo ambayo yanakuvutia. Subiri litakapokufika ndio uone sura yao ilivyo. Tatizo linapokufika utapenda ulipwe mafao yako mapema ili uweze kulitatua. Karaha unakuja pale unapoambiwa usubiri.
Wanalipa ila kama uko sloo wewe kuprocess unachotakiwa upande wako utajichelewesha mwenyewe na utawasingisia wao... peleka documents zote na sahihi na harala kama inavyotakiwa pale unapotaka kupata hayo malipo haraka..
 
Nionavyo Mimi, kampuni za Bima zina mitego mingi Sana. Pesa hazitolewi kirahisi namna hiyo. Wajanja Sana katika kutoa maelezo ambayo yanakuvutia. Subiri litakapokufika ndio uone sura yao ilivyo. Tatizo linapokufika utapenda ulipwe mafao yako mapema ili uweze kulitatua. Karaha unakuja pale unapoambiwa usubiri.
Umesema vema. Maana fikiria eti utoe 500 x 12 = 6,000/- kwa mwaka halafu ukifa ulipwe 1,000,000/-

Yaani 6,000 kwa mwaka yenyewe tu mpaka ifike 1,000,000/- ni miaka 167. Sasa hapo ndo umejiunga una miaka 40, halafu ufe kabla hujavuka miaka 70.

Wanasema mwisho wa kujiunga ni miaka 70, kwa hiyo ina maana ukifa baada ya kuvuka miaka 70 hautalipwa maana unakuwa ushapoteza vigezo vya uanachama. Kama ulichanga basi itakuwa uliwachangia wenzako watakaokufa kabla ya kuvuka miaka 70.

Hapo wameshapiga mahesabu na kugundua kuwa watu wengi wanakufa baada ya kuvuka miaka 70.

Kiufupi ni lazima watakuwa wasumbufu sana kwenye kulipa. Maana hakuna mtu anayeweza kuchanga mpaka kufikisha hata nusu tu ya hiyo hela ya fidia.
 
Back
Top Bottom