SHILINDE
Member
- Jul 23, 2010
- 14
- 6
Fundi Muashi yupo juu ya ukuta hata ANAMU hajafika, kasimama na ngazi, kashika mkono bawa na beseni la tope limeshakwisha mota. Vibarua na wasaidizi wa fundi wapo chini wamekaa wanabishana na kukosoa tu.... "fundi kapindisha ukuta...." .....hapanaaa amegeuza tofali.." hapana amezidisha mota...!" huyu fundi...hajui! masaa yanaenda.!
hakuna kibarua au msaidizi anaetoa mawazo mbadala ya nini kifanyike, au kukusoa kwa kujenga ili ujenzi uendelee.
ikifika jioni kazi haijaisha sidhani kama vibarua na wasaidizi watalipwa ujira kutokana na ubishi wao na kujionesha tu wanajua kuongea, kubishana na kukosoa..!
SIJUI NANI KATULOGA..?