Nani Hajui Kwamba Taratibu mzuri ni zao la Mgogoro Mibaya?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Ni Bahati mbaya kuwa; hapa Afrika, wengi wa watu hasa viongozi huichukulia migogoro kwa mtazamo hasi tu!
Wasijue kuwa migogoro huwa na upande wa pili ambao ni mzuri tu.

Nani hajui kuwa taratibu zote nzuri za kiutawala tulizonazo leo katika kujiamulia mambo yetu wenyewe, tena kwa uhuru ni matokeo ya migogoro mibaya iliyoanzishwa na wagipania uhuru wa ndani na nje ya bara hili.

Nani hajui kuwa taratibu zote nzuri za kurinda maslahi ya wafanyakazi, wakulima au wajasiriamali, zilizopo duniani sasa, ni matokeo ya uwepo wa migogoro mibaya mno ambayo iliwahi kutikisa huko nyuma!
Nani hajui kuwa hawa wazungu tunaowakubali sana wameweka utaratibu wa kuheshimiana baada ya kuwa na migogoro mibaya iliyowagharimu maisha ya wenzao!

Kimsingi wenzetu weupe siku zote wameitumia migogoro katika kupiga hatua mbele, wakati sisi weusi mara nyongi tunaitumia migogoro kupiga hatua nyuma!

Hebu fumbua macho yako uone hapa kwetu.

Tazama migogoro ya wakurima na wafanyakazi.
Tazama migogoro ya wawekezaji na wananchi.
Tazama mgogoro wa katiba mpya.
Kisha utazame migogoro ya vyama vya siasa mara baada ya uchaguzi.

Ndipo urudi kutazama migogoro ya mikataba mibovu ya uwekezaji katika sekta za madini.

Na kadharika na kadharika.

Sasa basi waafrika kama binadamu wengine wenye utashi iko haja ya sisi wenyewe kutengeneza taratibu nzuri ili ziwe majawabu katika migogoro yetu.

Vinginevyo, tukisubiri hawa wazungu ndio waje kutuwekea utaratibu mzuri wa kujiongoza basi tukubali kuwa sisi tuna mapungufu makubwa kuliko wao!
Mbona wao wameitatua migogoro yao kwa kuweka taratibu nzuri bila sisi?
 
Back
Top Bottom