matokeo haya ya form form 2012 ni nyongeza ya maswali juu ya maswali tuliyojiuliza zamani kuhusu nani msimamizi wa elimu nchini.Ni nani aliyepaswa kuhakikisha watoto wa shule zetu hasa hizi za walalahoi wanasaidiwa katika kuelewa masomo yao na hata kufaulu mitihani yao. Au aliyenacho ndiye atakayeongezewa?
ukiangalia kwa umakini, hakuna hata mmoja anayesimamia au mwenye moyo wa dhati kabisa kuona tunatoka huku tunasonga mbele.Hapa si serikali kwa maana ya rais ambaye pia huwateua mawaziri kusimamia ukuaji wa elimu nchini. Tunamwona Mulugo na Kawambwa ambao pamoja na kukabidhiwa jukumu hili hawajui waanzie wapi na waishie wapi; wamepwaya sana. Na wanapoelezwa ili wasaidiwe wao huwa wakali na kuwatukana watu, watu wanaona tu, na kama mmoja alivyopendekeza ni kuvuliwa dhamana na kuongoza.
Vile vile hata hizi dini pia hazipo hapo kusaidia mwanafunzi iwe ni kiroho ama kimwili, kwa kuwa wao pia -wapo kwa maslahi yao binafsi. pamoja na kuonekana kuwa shule zao zinafanya vizuri lakini ni kuwa wana pesa za kuendeshea shule; mfano waroman na saint schools zao; pesa ipo, na ndio maana wanaweza kupata vitabu vingi, walimu wazuri na chochote wanachotaka. ila ubaya wao, badala ya kwenda kuwasaidia watanzania huwachagua watanzania wenye nazo kwa maana hata karo zao kwa mtoto mmoja tu kwa mwaka unakuta ni mara mbili ya pato la mtanzania wa chini anayelipwa 80,000 kwa mwezi. lakini bado watoto hawa hubaguliwa ndani kwa wale tu 'cream' yaani vichwa ndio pekee watakaoweza kusoma hapo. kingine ni kuendelea kubaguliwa pia unapoonekana kulegalega katika masomo ili usije ukaiabisha shule yao na kuinyima mapato pale utakapofeli.
kwa hiyo ukiangalia kwa undani wake, sio serikali ama hawa wenye mashule binafsi ambao wako tayari kuona kuwa elimu inakua na watoto wetu wanafaulu vizuri na kuweza sasa hata kushindana na nchi nyingine dunaiani kwa kujiletea maendeleo wenyewe. kama kweli watu wa dini wote wangekuwa wakweli, wangejitahidi sana kwa pesa za sadaka na ushawishi wao kuwasaidia watanzania wote na si wale weney nacho-huu ni unafiki
Tanzania pia tunaongoza kwa kuwa na taasisi nyingi zinazojifanya kushughulikia elimu tanzania, mfano Mfuko wa elimu nchini, NGOs kama WAMA na EQUAL RIGHTs ST Marys na nyingine lakini zote hizi inaonekana kama ni usanii kwa kuwa hii mifuko haisaidii mtanzania yeyote bali hutunisha tu matumbo yao. ujanja hapa ni kuanzisha tu na misaada kibao inamwagika kutoka nje.
Watanzania tusipochukua hatua za dhati kuifufua elimu yetu, watoto wa walio wengi wataendelea kuwa mambumbumbu nakuendela kunyonywa na wachache. Teana huu mtindo wa kuegemea private schools ungeondoshwa kabisa, kwa maana sasa ya kurejesha hadhi ya shule zetu zinazomilikiwa na serikali. mfano mzuri walisema wataregulate ada zinazochajiwa na shule binafsi-miaka inakatika tu hakuna lolote; kumbe wale wanaotaka kuregulate ndio wamiliki wa shule hizo...Mambo ni mengi, bado nauliza ni nani anatakiwa kusimamia, ama nini kifanyike aibu hizi zisiendelee kutukumba huku tukipoteza rasmali- watu kubwa namna katika lindi kubwa la umaskni?nawasilisha