Habari za asubuhi jukwaa,
Nimeleta hii hoja jukwaani ili kupata mawazo na pengine kusaidia na wengine pia ambao wamewahi au watakutana na changamoto kama hii.
Hoja ya msingi. Jumamosi tukiwa safarini tulipigiwa simu na mmoja wa watoto wetu akieleza kuwa umeme umeisha kwenye LUKU. Suluhu ya haraka kwangu mimi ilikuwa nikununua umeme kwa njia ya Mpesa. Hivo kwa kutumia Mpesa nilituma shilingi Elfu tisa mia tano. (9500/=) Ujumbe ulirudi ukisomeka hivi LUKU2 MUAMALA HAUJAFANIKIWA, Amount too low, Your money will be reversed. Nikaona isiwe taabu nikawatumia watoto shilingi elfu 20, wakanunua umeme.
Issue kwenye kureverse ile hela, siku hiyo hiyo nikapiga simu vodacom huduma kwa wateja, mhudumu akanambia hela hiyo itarejeshwa ndani ya masaa 24, Jumapili ikapita, jumatatu nikapiga tena simu nikaambiwa hela itarejeshwa ndani ya siku saba.
Mpaka sasa kimya, nimepiga simu wananambia wanipe namba niongee na Tanesco kwa kuwa wao niwawezeshaji tu.
Swali kwa nini mimi ndo niingie tena gharama kupiga simu tenesco wakati transaction imefanyika kati yangu na VODA, VODA na Tanesco. Kama Voda hana uwezo wa kujua kuwa kiwango anacholipa mteja kupata huduma Tanesco hakitoshi, Tanesco anapopokea hela na kugundua haitoshi kwa nini asikate kiwango kilichopo na kumweleza mteja kuwa hela fulani imekatwa unadaiwa kiasi fulani badala ya kubaki na hela yote?
JE inatosha Voda kunambia mimi anipe namba ya simu nifuatilie hela yangu Tanesco? Ni hayo tu kwa leo. Karibuni wadau.