Zimpombe
Member
- Aug 9, 2016
- 28
- 24
Nimesoma maneno ya waziri mkuu sehemu nyingi anazopita na kuchagiza kuwa mwanasiasa atakaye thubutu kuvunja amani hatavumiliwa hata kidogo. Wananchi kwa hiari yetu, kwa upendo wetu na kwa ajili ya kuilinda Tanzania, tuliamua kuwa na katiba yetu, ambayo ndiyo dira yetu katika maisha yetu ya hapa nchini ya kila siku katika siasa, uchumi na kijamii.
Kitendo cha rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, ni kitendo kiovu kinacho hatarisha amani ya nchi yetu tuliyozoea kuwapokea wakimbizi kutoka jirani. Polisi nao wametereza kwenye mteremko ule ule wenye uterezi, nao wanapigilia msumari kwa kupiga marufuku mikutano ya ndani wakuhusianisha na kuuawa kwa polisi wetu juzi. Ili hali haya matukio yamekuwapo tangu kipindi cha mh. Kikwete.
Ningemshauli rais Magufuli, ya Kagame amuachie kagame, ya Nkurunzinza amuachie Nkurunzinza, na ya Museveni amuachie Museveni. Hawa wote wametokea msituni, lakini si kwa rais wetu, yeye amepita kwa karatasi, na hilo karatasi ni muongozo wa katiba. Rais huyu anafanya jambo la hatari ambalo marais wote waliopita hawakupata kuthubutu.
Nyerere hakuwa mjinga kuruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, hapo kamati ya Nyalali iliona 20% tu ndio walio hitaji vyama vingi. Lakini Nyerere aliwapa wachache, sio kwamba alipenda, hapana, wakati ulimlazimu, alikuwa hana nama. Ndipo sheria ya vyama vingi ikatengenezwa ili kuongoza vyama vingi 1995, na hii ndiyo iliyo ruhusu mikutano hii.
Kikwete hakuwa mjinga kuwafanya watu waongee na kuandika wanavyojisikia, wakati ulidai hivyo. Ukiwanyima watu kuongea, watatafuta namna nyingine ya kuongea, na hii ni hatari zaidi. Tukumbuke, mataifa ya magharbi huwa yanapenda kujipenyeza ktk chokochoko kama hizi na kuruga kila kitu. Amani hailindwi kwa makombora, bunduki, wala mabomu. Amani hulindwa kwa upendo, majadiliano, haki, na sheria ambazo kila mtu yupo chini yake. Rais Magufuli aige mfano wa Uhuru Kenyatta, anacheka na upinzani, wanakaa meza moja kuongea kwa ajili ya kulinda mustakabali wa amani ya nchi yao.
Naamini maneno ya Jenerali Ulimwengu kuwa, kidemokrasia tumerudi nyuma kwa miaka 50 tena. Hivyo waziri mkuu kusema mwanasiasa atakaye vuruga amani, hapana. Anae vuruga amani ni yule anaye vunja katiba. Tuna Tanzania moja tu, tukiiharibu hii, hatutakuwa na mbadala, hivyo wanao mshauri rais, wamshauri sana kuhusu katiba ambayo aliapa kulinda kuitetea.
Mungu ibariki Tanzania.