a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,966
- 2,200
2 Nya 7:14
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
***UNYENYEKEVU unapokwenda mbele za Mungu kuzungumza naye.
****USIJIHESABIE HAKI
fahamu kuwa hatukustahili ila ni NEEMA yake na upendo wake,na huruma yake tu.
Luka 18:10-14
Neno: Bibilia Takatifu
10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’
14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”
UKIJIHESABIA HAKI na kujiona unastahili mbele za Mungu unakuwa unaharibu kwa sababu tunaokolewa kwa NEEMA sio kulipia gharama au tunajiokoa wenyewe kwa uweza wetu .
***TOBA kutubu makosa yetu na kuomba rehema,tujione hatufai mbele za Mungu hatuna wema wa kutosha kujiosha dhambi zetu ila damu yake Yesu ,gharama ALILIPA DENI YETU kwa gharama ya mauti,msamaha wa dhambi tuliupata kalivari.
2 Wafalme 20:1-6
2 Wafalme 20:1-6 BHN
BHN
SUV
Neno
SRUV
Wakati huo Hezekia aliugua sana karibu na kufa. Ndipo nabii Isaya, mwana wa Amozi alipomwendea na kumwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu; ‘Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.’” Hezekia akageukia upande wa ukuta na kumwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi ukumbuke jinsi nilivyokutumikia kwa uaminifu na kwa moyo wangu wote na kutenda yaliyo sawa mbele yako.” Hezekia akalia kwa uchungu sana. Lakini kabla Isaya hajapita ua wa katikati, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia, kusema, “Rudi ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wa Mwenyezi-Mungu: Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu yako Daudi, nimesikia ombi lako na nimeona machozi yako. Nitakuponya na baada ya siku tatu utakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Nitakuongezea miaka kumi na mitano ya kuishi. Nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mikononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu kwa ajili ya heshima yangu mimi na kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi.”
Kuomba toba wengine hutoa mpaka machozi ya toba wakijutia moyoni dhambi zao na kutubu.
pia baada ya kutubu dhambi na kusamehewa inakupasa KUZIACHA usitende dhambi tena.
****PELEKA HOJA ZAKO mbele za Mungu sio malalamiko,manun'guniko.
Isa 41:21
Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.
Isaya 43:26
[26]Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
peleka hoja mfano zako mfalme alikuwa ameandika hoja zake katika UKUTA au daftari lake au kumbukumbu zake ,hivyo alirudi kipitia kumbukumbu zake alizoandika akamkumbusha Mungu akumbuke ,wema wake alioutenda ,na jinsi alivyomtumikia Mungu,
hoja nyingine ni kutumia NENO neno lake na ahadi zake kutoka katika neno lake.
*** IMANI ISIYOKUWA NA MASHAKA
a)imani ya kupokea muujiza wako kutendewa
b)imani katika kuomba
Mt 8:8
Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
akida alikuwa mnyenyekevu,hakujihesabia haki,alijiona hakustahili,alikuwa na imani ya KUPOKEA.
Mk 11:24-25
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 2
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Amponya Mtu Aliyepooza
3 Wakaja watu wanamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4 Waliposhindwa kumfikia Yesu kwa ajili ya msongamano wa watu, wakatoboa tundu darini, wakamshusha ndani yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.
5 Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Mwa nangu, dhambi zako zimesamehewa.
AKAMPONYA aliyepooza
Alipo ona IMANI yao.
Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda.
“Matendo 14:9-10.
Mtu huyu hakuombewa,wala hakuwekewa mikono bali alilisikia neno la Mungu lenye uweza lililokuwa likihubiriwa na Paulo,kisha alipoonekana ana imani ya kuponywa~aliambiwa asimame na aende zake,maana uponyaji ulikuwa ni mali yake,sababu aliamini.