simba songea
JF-Expert Member
- Feb 8, 2016
- 1,498
- 1,214
Ndugu habari zenu nafiri wazima wa afya. Leo ningependa tujifunze namna ya kuishi maisha yenye uhusianao. Maisha ya uhusiano ni ile hali ya maisha ya mtu kuhusiana na mfumo mzima wa mwili wake au kuendana na mazingira anayoishi. Watu wanagombana na majirani zao kwa kushindwa kuishi maisha ya uhusiano.
Zifuatazo ni hoja ambazo zitasaidia uishi maisha ya uhusiano;
1. KUWA WEWE;kama kweli unataka uishi maisha ya uhusiano huna budi kuwa wewe, hapa inamaana kwamba uwe na tabia zako halisi na si za kuiga.
2. PUNGUZA KELELE; binadamu wengi tumekuwa ni watu wa majivuno utakuta ukifanikiwa kidogo unaanza maringo na kutangazia watu mali zako sasa hizo zote zinaitwa kelele kwa maana kelele ni part ya uchafu yaani unwanted materials katika maisha ya watu.
3. KUWA MWEMA; Utajiuliza nawezaje kuwa mwema, mwema ni mtu ambaye 'ANAKUMBUKA MEMA YOTE ALIYOFANYIWA NA MABAYA YOTE ALIYOWAFANYIA WENZAKE' wakati mtu mbaya ni yule 'ANAKUMBUKA MABAYA ALIYOFANYIWA NA MEMA YOTE ALIYO WAFANYIA NA WENZAKE'
4. UAMINIFU WA MAPENZI; hili uweze kuishi maisha ya uhusiano lazima uwe mwaminifu katika mapenzi. Usiwe tapeli wa mapenzi kwa kumuambia mwenza wako unamwona kwenye glass ukinywa maji. Mtu mwenye mapenzi ya kweli hawezi kumwambia mpenzi wake 'nakupenda sana' kwa maana tuna amini kwamba upendo wa kweli unatoka moyoni na sio mdomoni pekee.
5. FANYA MAZOEZI; hiki kitendo ni kizuri kwa afya maana unakuwa na afya njema pia iliyo imara, mbali na hayo pia kitendo cha kufanya mazoezi pindi utoapo majasho hayo tunasema ni maumivu uliyohifadhi katika mwili wako. kwa hiyo yanatoka kwa njia ya majasho.
6. KUWA MKWELI; math 5;33 umeeleza kwa kina. Unajua watu wanashindwa kuelewa kuwa ukweli ndio dawa ya ushindi katika maisha yao, huwezi kufanikiwa kama una tabia za uongo. Mtu mkweli siku zote anakuwa na amani katka moyo wake kwa maana anakuwa haifadhi furushi la uongo katika moyo wake.
7. PUNGUZA STAREHE; unatakiwa kupunguza au kuacha starehe. Kama umeshindwa kupunguza basi acha na kama umeshindwa kuacha basi hilo tatizo. Nakumbuka nikiwa mwanafunzi IFM natoa presentation darasani niliposema hili neno wanafunzi wakacheka sana nikawaambia binadamu hatuishi kwa starehe bali kwa tarehe.
8. JALI MUDA; unatakiwa kuwahi muda kabala muda hauja kuawahi, muda siku zote haujirudiaa yanajirudia masaa tu tena kwa vipindi tofauti. Tusiishi kwa mazoea kwa maana mazoea huzaa umbea. Maisha tuliyo nayo ni mafupi mno kama umeshindwa kujiandaa angali kijana usitegemee utafanikiwa uzeeni.
Kwa maana binadamu tumeumbwa kama gurudumu la gari kadri linavyo tumika ndivyo linavyozidi kuisha. Mfumo wa maisha ya binadamu kama duara unapoanzia ndipo utakapo ishia, maisha ya binadamu ni fikra anaishi tangu akiwa tumboni kwa mfano,mtoto mdogo anapozaliwa anasaidia kila kitu kuanzia kula mpaka kuvalishwa baadae anakuwa mtu mzima anajitegemea. Baadae anazeeka anarudi katika hali ya mtoto mchanga kuanzia kulishwa had kuvishawa. Mwisho wa siku anakufa anarudi alipo anzia, hapo sasa ndo tunasema maisha ya binadamu kama duara.
9. FANYA KAZI; mtu anaheshimika sio jinsi alivyo bali kutokana na kazi yake anayofanya. Unaweza ukawa unavutia kimuonekano lakini hukakosa kuheshiwa na jamii yakoo kutokana huleti mahitaji nyumbani, hapo hakuna atake kuheshimu. Hata muuza machungwa barabarani anaheshimika kutokana na biashara yake anyofanya.
Nimalizie kwa kusema siku zote washindi hawakati tamaa wanaokata tamaa sio washindi. Kama umeshindwa kupata unachokipenda penda unachokipata, hiyo ndo ngazi ya kufikia unachokipenda. Nashukuru kwa kusoma na Mungu awabariki....