Japo mimi sikupata hiyo One, ila naamini siri ni kusoma tu, plus:
1. Gawa muda nusu nusu, yani nusu ya kupiga msuli yatima na nusu ya kupiga na masela kama ni wa class kwako, tuition nk.
2. Usilale sana, ukiachilia mbali ma'genius, sisi wa akili za kushake well before use lazima ukeshe hapo. Kwa siku ukilala masaa matatu inatosha sana.
3. Uwe na siku za kula bata. Mfano weekend refresh mind, ubongo ukae sawa.
4. Kama unamuamini Mungu, omba sana.
5. Vitini vya great teachers vinasaidia pia. Kina Unga, Muddy, Ngaiza, Mgote na wengine niliishawasahau maana kitambo, hakikisha hakuna topic unashindwa kuielewa, elewa kila kitu hata kwa kuuliza ka wengine.
6. BAM huwa inakamata wengi pia, hapo usicheze mbali na watu wa PCM na EGM kwa msaada wa hesabu.
7. Pitia sana past papers za necta na mashule mengine, hakikisha hakuna swali linakosa jibu. Usilale bila kupata jibu.