Nakutia moyo: Furahi siku yako ipo na hicho kinachokunyanyasa kitalia siku hiyo

majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,351
4,029
Mpenzi msomaji,

Popote ulipo Duniani

Nakusalimu katika nia njema kabisa ya kukutia moyo.

Kwa mfano huu! pokea faraja kwa kila gumu unalopitia. Daima kumbuka kwamba tuliumbwa na Mungu na Mungu wetu anatutakia yaliyo mema na yeye hutuandalia njia ya kuondokana na maumivu yoyote tunayotendewa na wengine.

Kama wewe ni mfanyakazi na unanyanyasika sana na boss wako, jipe moyo kuna siku manyanyaso yataisha, ataondoka tu hapo alipo na kukuacha wewe unaendelea kufurahi. Hata kama huyo boss anajiona ana nguvu kiasi gani, anaushawishi kiasi gani, ana uwezo wa kufanya lolote one day atakuwa mdogo kama piriton na wanyonge tutashangilia.

Siku ya bwana, siku ya ukombozi ikifika utafurahi hata kama ulidharauliwa hadharani, utacheka hadharani.

Nina Boss wangu hapa mnyanyasaji namwambia iko siku. Nakutia moyo na wewe kwa mfano huu furahi siku yako ipooo na hicho kinyanyasaji kitalia siku hiyo.

Toa mfano wako tufarijiane hapa.
 
Pambana ili nawe uwe boss, usipambane kuomba boss aanguke maana hata akianguka haikufanyi automatically na wewe uwe boss!
 
Back
Top Bottom