Hashim bin Faustin
Senior Member
- Jan 30, 2017
- 177
- 216
NA MPONGEZA MAKONDA ZAIDI YA KUMLAUMU
Ndugu wanajamvi, napenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza Ndugu yetu Mkuu wa Mkoa wa DAR Mh. Makonda, kwasababu zifuatazo ,
Ni kijana ambaye amezaliwa kutoka kwenye familia masikini na duni kabisa lakini kwa uvumilivu na uhodari wake kafanikiwa kufikia hapo alipo hivi sasa. kwa hakika hakuna binadamu anakosa mapungufu katika maisha yake lakini inategemea na aina ya mapungufu ya kila mmoja wetu na jinsi kila mmoja wetu anavyo weza kupambana na mapungufu husika. Huyu ni kijana aliye zaliwa toka familia masikini lakini kwa ujasiri wake ameweza kupambana na kufikia hapo alipo hivi sasa.
Hata kama njia aliyo tumia ina walakini wowote cha Msingi ni kutizama lengo lake na je lilikuwa ni nini ?, kwa hakika kijana huyu toka familia masikini. Amepitia katika maisha magumu sana tena sana na ameweza kuvuka vikwao vingi sana hadi kufikia hapo alipo. Lazima tumpongeze.
Hivyo kugushi na kutumia cheti cha mtu mwengine ili kupata nafasi uweze kujiendelea kielimu kwa kuzingatia mazingira ya umaskini aliyokuwa yana mkabili Kijana huyu kwa kipindi anatenda kosa hili (kama kweli) kangu mimi nina msamehe na ninafungia macho kosa hili kabisa wala sihitaji kujadili uhalali wa elimu yake bali ninachoangalia hivi sasa ni matendo yake baada ya kupata elimu husika na nafasi ya uongozi katika jamii yetu , na hapo ndipo nampa angalizo na sitomsamehe akitenda sivyo ndivyo. Naomba ileweke ndugu zangu katika Taifa letu wamepita viongozi wa aina nyingi na WAMESOMA KWA VIZURI SANA NA WAMEISHI KATIKA MAISHA MAZURI muda wote wa maisha yao lakini kiutendaji na nidhamu katika uongozi wao umekuwa mbovu na wa ovyo kabisa. Hivyo tuachane na kufukuwa makaburi ambapo kwa historia ya Nchi yetu tutajikuta tunajikwaza sisi wenyewe na kijirudisha nyuma.
MATENDO NDANI YA UONGOI WAKO! !
Hapa ninakulaumu sana kwani umekuwa ukitekelea wajibu wako kama vile wewe ni mfalme katika jamii yetu umejitia umalaika na kujiona wewe ni mtu safi usiyekuwa na doa umesahau umasikini wako na kuchaguwa marafiki wapya wenye majina mkubwa na mkwanja mnene , hapo hapo umekuwa ukishirikiana na makundi ambayo mimi binafsina naweza kuyaita ya kihalifu ili kufanikisha mambo yako katika uongozi wako. Nasema hivi kwasababu yamesemwa mengi sana kuhusu hawa washirika wako katika jamii yetu tokea uongozi wa awamu ya 4 na hadi hivi sasa bado yana semwa mengi. Lakini umekuwa karibu na hawa watu kama alivyo kuwa baba yako aliyetangulia mbele ya haki ‘Mola amsamehe mazambi yake na amuhifadhi kwa Amani huko peponi kwa kadiri Mola apendavyo’ Ameen. (nasema hivi kwani wakatia wa uhai wake niliona picha wakiwa kwenye Ndege na mmoja wa halifu hawa wakienda au toka majuu pamoja) kiongozi kama wewe mwenye sura ya kiwana Mapinduzi na ukiwa unalengo zuri katika uongozi sitegemei kukuona ukishirikiana na makundi kama haya !! ungeya epuka na kukaa nayo mbali kama ukoma ... ! hata kama ni wafadhili wako wakubwa, hatuhitaji michango ya watu waliotuliza miaka yote na kusababisha umasikini mkubwa katika Taifa letu na kusababisha kina mama na watoto vijijini wanakufa ovyo kwa kukosa huduma bora za afya na elimu yetu kuwa duni..wakati wao wanaishi maisha ya kifalme kwa pesa walizo tuibia huku tunatizama kwa macho yetu. Wajinga ndiyo waliwao......!!
Ndugu Makonda napenda uelewe sisi Watanzania wa kizazi cha ayati Baba wa taifa NYERERE ! tuna sifa yetu moja nayo ni hii “ SISI NI MASIKINI JEURI” Hatuhitaji kuwakumbatia wezi wa rasilimali zetu eti tu kwasababu wanaweza kutumia pesa zao chafu kutusaidia na kutulaghai, Mh. Makonda naomba uelewe sisi Watanzania Masikini tuliichukia CCM kwasababu ya kuwakumbatia Matajiri na kutusahau sisi Masikini wa kitanzania hivyo basi unapokumbatia matajiri wale uwapendao wewe na huku ukitulamba kisogo nyuma yetu na huku ukiburuza chogo mbele yetu sisi Masikini wa taifa hili hatukuelewi kabisa na hatutakubali ujinga huu. Sisi masikini na Wazalendo wenye uwelewa kidogo kwa mambo yanayo endelea hatuwezi kukaa kimya kamwe tutapiga kelele kila kukicha na hatuta nyamaza kamwe na utabakia na masikini wachache watakushangilia na watafanya hivyo kwa njaa zao au kwa ufinyu wa kuelewa wao.
WEWE UNASURA ZOTE ZA WANA MAPINDUZI FANYA MAPINDUZI YA KWELI KATIKA JAMII YAKO ! JENGA TAIFA LENYE USAWA NA HAKI ILI KINA "DAUD BASHITE" WA LEO WAPATE NAFASI YA KUJIENDELEZA BILA KUFANYA ULAGHAI WA AINA YOTE.
Vita ya Madawa ya Kulevya !!
Hapa umesimama kupambana na hili janga la Taifa ambapo vijana wengi wanateketea kwa kubwia unga. NAKUPONGEZA, Lakini vita yako imekosa hekima na Busara na imejaa Usanii. Huu ndiyo ukweli. Jipange upya katika hili kwani kelele za kwenye majukwaa haziwezi kukusaidia cha muhimu simamia vyombo vya utendaji vifanye kazi yao kwa haki na bila uonevu wowote. SIMAMIA HAKI NA IWE HAKI YA KWELI TU SI YA KUTENGENEZA. Elewa M'Mungu ni wetu wote na wote tuna muomba na tuna mtegemea yeye TU.
NAKUTAKIA KAZI NJEMA NA MAFANIKIO KATIKA KAZI ZAKO ZA KILA SIKU
MWENYEI MUNGU AKULINDE NA KUKUONGOZA KWA KUKUPA BUSARA ILIYO KAMILIKA.
WASALAAM.