Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Kwako mheshimiwa Rais
Mimi binafsi kama Mtanzania, naridhishwa sana na utendaji wako wa kazi katika kutuhudimia sisi watanzania
Moja ya taifa lenye watu wavivu sana hapa dunia,uvivu wa kila kitu mpaka kufikiri
Binafsi nimefuatilia baadhi ya hotuba zako katika mikoa ya Kagera, Geita, Simiyu na Shinyanga
Ni hotuba zenye kutufanya sisi raia wako tujue unataka kutupeleka wapi
Imekuwa ni hulka ya sisi watanzania,katika kutaka kuararisha uvivu wetu,kila inapototea tatizo au maafa kila mtu utaka kupewa msaada na serkali
Mfano katika tetemeko lililotokea mkoani kagera, naomba kutoa pole kwa wahanga wote wa tetemeko hilo,Mungu awapumzishe kwa amani waliopoteza maisha na kuwapa nguvu wale wote waliopoteza ndugu au mali katika janga hilo
Lakini pamoja na yote hayo, tetemeko hilo lisiwafanye wana kagera wakalitumia kama kisingizio cha kupewa chakula ama kutaka kujengewa nyumba, huo ni uvivu kama ilivyo ada kwa sisi watanzania, ni aibu kwa mikoa kama kagera, Geita ama Mwanza kusema eti kuna njaa kisa kuna upungufu wa mvua, eti waletewa chakula na serikali
Wakati mikoa hiyo imezungukwa na ziwa kubwa na mito mingi,kwa nini wasibadili mawazo na kujua wanaweza kufanya kilimo cha umwagiliaji?
Kwa sababu tulishazoea huko nyuma, matatizo kama hayo serikali iligawa chakula bute
Hilo haliwezekani, kama taifa inabidi tubadili fikra na mawazo na mtazamo,tatizo kubwa la sisi watanzania ni UVIVU
Ukiwasikiliza wanasiasa unaweza kusema wana huruma sana na wananchi, kumbe ni upuuzi tu wa kutaka kuwatumia wananchi wenye matatizo katika kutafuta huruma zao, ili waweze kuja kushika dola
Mheshimiwa Rais nakuomba tena kwa msisitizo mkubwa, naomba ulitangazie taifa lote kuwa ninyi kama serikali hamtatoa chakula cha bure kwa yeyote yule, hii itadaidia watu kubadili mawazo na kuanza kufanya kazi kwa bidii au kutafuta njia mbadala kama kulima mazao ya muda mfupi na yanayoweza kuhimili ukame,
Kama ni yale maeneo ya wafugaji, wanaweza kujipanga na kubadilishana mifugo yao mingi isiyo na tija na kupata chakula,kutoka katika maeneo mengine yenye chakula cha ziada
Watanzania tumefikishwa hapa na wanasisa, ambao siku zote hawataki kusema ukweli kwa kuogopa kukosa kura kutoka kwa wananchi, ukiwaona wakiongea unaweza dhani wana huruma ama kujali sana wananchi,kumbe ni uroho tu wa madaraka na kutaka kujinufaisha wao na matumbo yao
Kwa wanasisa wenye nia njema,kipindi kama hiki kilipaswa wawe wanazunguka vijijini na kujaribu kuwaelimisha wananchi ni njinsi gani ya kukabiliana na ukame, ambao ni tishio la dunia yote kwa sasa
Nakupongeza sana mh Rais kwa kuwa muwazi na mkweli katika hili, pasipo kuogopa kukosa kura katika uchaguzi 2020, wengi hawawezi kukuelewa kwa sasa, hii ni kutokana na historia yetu huko nyuma,ya kuzoea vitu vya bure bure na uvivu uliokithiri, Lakini katika siku zijazo wengi watakuelewa na kukushukuru