Nakosa raha nisaidieni

Chiriku

Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
47
Reaction score
8
nilikua na mpenzi wangu ambaye tulipendana sana, lakini ilitokea kama bahati mbaya mawasiliano yakakatika gafla kama miezi 3, kila nilipojaribu kufanya mawasiliano nae alikataa kabisa kupokea simu, ila kwa bahati nzuri au mbaya tumejikuta tunafanya kazi kampuni 1 lakini kwa bahati mbaya tayari ameshajikita ktk mahusiano na mtu mzima (yaani jimama) aliemzidi umri miaka 12. sasa nakosa sana raha kwani nampenda sana na sielewi kama bado ana wazo lolote juu yangu ndio bye bye. ushauri wapendwa wangu
 
Haikutokea bahati mbaya Mawasiliano kukatika ghafla. ALIKATISHA MAWASILIANO MAKUSUDI. wake up girl!!!
 
manafanya kazi pamoja na kampuni moja, mnafanya mawasiliano hataki hapokei simu...! sijaelewa ila tulia endelea na kazi wacha ale pesa za huyo gamba...
 
He ya nn kujiweka roho kama tai??
Jifanye hujui chochote baina yako na yeye;;
Tatizo la wadada wengi huingia ktk uhusiano mzima mzima.
 
Inamana hujui kusoma hata picha? Aah embu jiongeze!! We mtu kakuchunia miezi 3 upo tu umeng'ang'ana, ANAROHO YAKO??? binti jitambue!! Mwenzio keshapata wakumlea na karibuni ataanza dozi ya ARV,upo?? Kampuni moja! Kampuni moja! Utakosa vyote! Achana na habari zake!!
 
kama bado unampenda na unamwitaji na unaamini aliyenae si sawa wewe ndo sahihi basi mwite umweleze nini kilichoko akilini mwako
 
somethings are too damn obvious. Move on!
 
mwenzio kapenda muache a fight for her love
 
pambana wewe dada umrudishe,wewe utakua nyumba ndogo hilo jimama pesa litakua BIG HOUSE no wivu hapo,kila mtu anakula chake kivyake!!
 
achana nae kwanza anaonekana ni mwanaume mvivu. me hapo ingekuwa tayari namwona kimeo kwa sababu ya kutembea na jimama kwa sababu anapenda kulelewa loh!!
 
mwenzio kapenda muache a fight for her love

mwekundu which love mwanaume mzembe huuyo wa nini? atafute wanaume wakakmavu wanaojielewa.. huyo ajielewi kabisa mwanaume unalelewa si sawa!
 
Ukitaka kujua kwa nini hakutaki tena, tafuta mwanaume uliyemzidi miaka 10.
 
Hakupendi.....chapa lapa,kampenda huyo jimama.Watu wakingonoka na jibaba sio inshu ila jimama ndo inakuwa balaa.
Check n balance!!!!
 

Raha jipe mwenyewe Chiriku..........akilizake changanya na zako.........Hao wanaokosesha raha wenzao Wapigwe tu, tumeshachoka sasa.
 
Omba ushauri kwa Wema Sepetu yeye ndio professional wa kurirudisha buzi lililokata kamba.
 
bidada embu angalia ustaraabu mwingine utapata wako atayekupenda kwa dhati, na siku ukiwa nae utaanza kusikia samahani naomba turudiane ni shetani alipitia. pole mwaya kupigwa kibuti noma siku nyingine uwe unawahi kupiga kibuti wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…