Nakerwa na tabia ya presenters kukodoa macho nje ya camera wakati wakiwa live!

kp kipanya44

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
10,709
13,152
Moja kwa Moja kwenye mada.., wengine huenda ikawa ni ngumu kuelewa,hii tabia ninayozungumzia hapa ni Ile Hali ya presenters wa tv stations,hasa akiwa anaongoza kipindi Cha taharifa ya habari,kuonekana amekodolea macho upande mwingine wa luniga mara tu report ya mwandishi flani inapoisha

Hii Hali nimeiona sana Star tv na chanell ten kwa mujibu wa kautafiti kidogo nilikofanya.., kiukweli huwa inanishangaza sana kwa presenter kukodoa mimacho kama mshamba flani hivi, utafikiri ni mtu wamemtoa kijijini kazulamimba huko na kumuweka kwenye chumba Cha habari

Nimefuatilia kwenye media zinazojitambua kama aljazeela huwezi kuona Hali hii,yaani huko report flani tu inapoisha ,macho ya presenter tayari yanakuwa kwenye camera! (Kwa watazamaji) huwezi kuona presenter akishangaashangaa report flani iliyoisha kama hapa bongo!

Nafikiri sisi watazamaji ndio tunafaa angalau kuonyesha ushambaushamba lakini sio presenters!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Huwa wanaangalia tv upande wa ili wa studio kuona reporter anavyorepot..akimaliza.kureport huwa anageukia kamera ya mbele...

Wenzetu..haswa hizo international media...wako more advanced sana kwenye vyombo...unakuta hapo hapo kwenye kamera ya kumchukua presenter Kuna kuwa na screen pembeni yake ya kumuonyesha namna naavyoonekana kwenye tv za watazamaji...so inakuwa rahisi Kwake kujipose vyema..

Pia wenzetu studio zao ni kubwaa sana..unakuta makamera yamemzunguka presenter Kila Kona...so hata kama atagueka wewe huku unayetazama utamuona vile vile

Huku sisi now baadhi ya media wameongeza kutoka kamera moja kuwa mbili Kwa sasa
 
Barikiwa sana mkuu,Ina maana kwenye hizo advanced media hata aikigeukia upande wa pili bado tu ataonekana amefocus kwa watazamaji!

Nimejifunza kitu

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom