Najiuliza Urais ungefaa nini UKAWA?

Najiuliza Urais ungefaa nini UKAWA?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Kwa picha hii ya bungeni Dodoma ni wazi kwamba bora tu hao jamaa wachukue urais kwanza ili UKAWA ujipange kuweka uwiano wa wabunge pale bungeni. Kama sheria zote pamoja na sheria mama na mapendekezo yote muhimu vinapitia bungeni, halafu ccm wana wingi wa wabunge ni wazi wasingependa kuona mswada unaoletwa na UKAWA unapita.

Mbaya zaidi waziri mkuu angetokana na ccm tu hivyo kuleta mtifuano bungeni na serikalini. Mwisho wa siku Rais Lowassa angeamua kuwa dikteta maana hakuna ambalo angelifanya bila kukutana na vikwazo. Hiyo ingepelekea UKAWA kuchukiwa na wananchi kwa kupandikiza udikteta. ccm wangechukua fursa hiyo kushitaki kwa wananchi pamoja na kwenye jumuiya za kimataifa.

hiyo pia ingesababisha UKAWA kupoteza mvuto kwa wananchi na kubwagwa vibaya uchaguzi wa 2020. Hayo ni maono yangu.

La msingi ni kuona ni jinsi gani bunge linakuwa na uwiano kwanza, mengine baadae
 
Kwani hamjui wabunge wenyewe wa ccm kama wamepita kwa uchakachuaji for a large percent? Msijifanye hamujui ukweli, wizi usingefanyika ccm insingefikisha wabunge hata 50 na huo ndo ukweli japo najua nyie ccm mtapinga tu kwani ukweli unauma...

Shame on you! !
 
Ukawa watabaki hivyo walivyo mpaka siku akiondolewa Mbowe
 
Kwani hamjui wabunge wenyewe wa ccm kama wamepita kwa uchakachuaji for a large percent ?
Msijifanye hamujui ukweli, wizi usingefanyika ccm insingefikisha wabunge hata 50 na huo ndo ukweli japo najua nyie ccm mtapinga tu kwani ukweli unauma...

Shame on you! !

Kwani wabunge wa Chadema hawakuchakachua Na hoa mnaowahonga viti maalum Na huku bado ni wafuasi wa CCM?
 
Matokeo ya ubunge Yakut an gas wa chini ya mtutu wa bunduki, alafu unawalaumu wapinzani badala ya kuilaani tume na ccm , baraza LA mawaziri limevunjwa siku ya kumwapisha raisi wa ccm, baadhi wapinzani walikuwa wanashindana na mawaziri, time yote ccm type watendaji wote ccm , hats hao wabunge was upinzani waliotangazwa ni kwa mbinde
 
Kwani hamjui wabunge wenyewe wa ccm kama wamepita kwa uchakachuaji for a large percent ?
Msijifanye hamujui ukweli, wizi usingefanyika ccm insingefikisha wabunge hata 50 na huo ndo ukweli japo najua nyie ccm mtapinga tu kwani ukweli unauma...

Shame on you! !
Sasa kifanyike nini? Ni wabunge wangapi wa ukawa kwa sasa wanapinga matokeo mahakamani? Nami naongea kama mwana ukawa
 
Ni kweli UKAWA wakajipange kupata wabunge wengi zaidi huku wakichukua tahadhari kutokuweka mgombea atakayewaombea kura wagombea wa CCM,kama alivyofanya mgombea wao aliyeshindwa( huku akidai kwamba ameonewa).Tunakumbuka mara kadhaa alisikika akiwaombea kura wabunge wa ccm mfano kule mkoani Mara(sina hakika kama ilikuwa ni kukusudia au kughafilika).
 
Kwani hamjui wabunge wenyewe wa ccm kama wamepita kwa uchakachuaji for a large percent ?
Msijifanye hamujui ukweli, wizi usingefanyika ccm insingefikisha wabunge hata 50 na huo ndo ukweli japo najua nyie ccm mtapinga tu kwani ukweli unauma...

Shame on you! !

Hao wabunge wa ukawa walioshinda ndo wameiba pia au ndo wababe, kwani ile idadi ya madiwani 1020 kwa 200 imetoka wapi. Huo ni ushabiki wa mihemko na siyo fact
 
Kwani hamjui wabunge wenyewe wa ccm kama wamepita kwa uchakachuaji for a large percent ?
Msijifanye hamujui ukweli, wizi usingefanyika ccm insingefikisha wabunge hata 50 na huo ndo ukweli japo najua nyie ccm mtapinga tu kwani ukweli unauma...

Shame on you! !

Mtaisoma namba maana mnaeleweashwa hamtaki sikia.
 
Sasa kifanyike nini? Ni wabunge wangapi wa ukawa kwa sasa wanapinga matokeo mahakamani? Nami naongea kama mwana ukawa
Raia Fulani Kungekuwa na ''uwanja sawa'' kwa vyama vyote kwenye uchaguzi Lowassa angeshinda! Na kama Lowassa angeshinda ndio ungeshangaa jinsi wanasiasa walivyo vigeugeu kwani wabunge wengi wa CCM wanamkubali na kumpenda Lowassa.

Hivyo nina uhakika asingepata shida kutawala. Na Lowassa angeshinda ni kuwa CCM ingeanza kudhoofu na hatimae ife kabisa kwani kinachoiunganisha sasa hivi ni nguvu ya dola tu!

Ina maana vyombo vyote vya ulinzi na usalama vingekuwa chini ya UKAWA (soma Lowassa) hivyo kwa kutumia hivi vyombo wale CCM ambao wangeleta kimbelembele wangesambaratishwa kwa muda mfupi sana!
 
tunarudi palepale kwenye ubabe na udikteta. Sidhani kama ccm wangekuwa laini hivyo kukubali tu kisa Lowassa Rais, mkuu. Hata Zanzibar imetuacha mbali kwa suala la mwamko na mabadiliko.

Pia tujifunze toka nchi ya Maynmar/Burma kuona ni jinsi gani Dola inaweza kuhama toka chama tawala kwenda upizani. Gonga hapa
 
Kwa mawazo Yangu nadhani tutakuwa na bunge zuri sana safari hii na wanaokalia kiti cha spika wasipoacha upendeleo ngumi zitapigwa bungeni safari hii
 
CCM ni wale wale. Tumemsikia pia Ndugai akitema cheche zake kwamba hatavumilia tena yaliyotokea. Hivyo tusubirie vimbwanga
 
Back
Top Bottom