Salamuni wanaJf,
Kama rais mtaraji wa Tz (2030), natanguliza pole kwa watz wote kwa vifo vya wapendwa wetu mabalimbali vinavyotokana na ujinga, umaskini na maradhi. Naumia sana moyoni mwangu ninapoona nchi yangu inaharibiwa mbele ya macho yangu.
Naangalia kwa undani sana jinsi ya kuondoa utando wa kutojiamini akilini kwa watz, hasa wale wailoenda shule. Utando wa kutojiamini umewafanya watz wengi kunung'unika na kufikiri kazi ya kuleta mabadiliko sio yao ila ni ya viongozi wa jamii.
Sikatai, viongozi wanatakiwa wawe sehemu ya usimamiaji wa maono ya taifa. Lakini labda tujiulize swali hili la kawaida sana ambalo kwa hali halisi pengine haliwezekani.
Je kama kila mtz angekuwa kama wewe, nchi yetu ingekuwaje? Kwa maana nyingine tunaponung'unikia ubovu wa utawala, mmomonyoko wa maadili, udhaifu katika michezo, ubabe wa dola, ufisadi, ubinafsi, zinaa, uongo, uvivu, tamaa ya uongozi, ubabaishaji, ugandamizaji, ubaguzi, uchochezi, unafiki, uchakachuaji, uropokaji, nk; wajibu wako ni upi katika kukomesha au kukataa hali hizo?
Mimi kama rais mtaraji wa 2030, nimejipanga sawa sawa. Sio tu kwamba nayatamka mambo hayo, au kuyachukia, au kunung'unika, bali nachukua hatua ya kuanza kujijenga kimaadili na kimtazamo ili hayo niliyotaja yasionekane hata kwa harufu maishani mwangu.
Tanzania mpya, huru, ya amani na baraka imezaliwa. Mimi nimeanza kutekeleza uzalendo kwa kujiahidi kwamba nitakuwa muadilifu mbele zangu mwenyewe, jamii yetu na mbele za Mungu.
Kama wewe unania kama yangu, karibu tuahidi pamoja, na kama ulikuwa bado hujafikiri hivyo fahamu leo ndio siku ya kujiwekea ahadi hiyo ya uaminifu na kuitekeleza. Tukifanya hivyo, mwaka 2030, tutakuwa na watu wasiopungua milioni 10 kati ya milioni 60 (kadirio la idadi ya watz mwaka 2030) waadilifu kwelikweli (kama wewe utafanikiwa kumuelimisha ingawa mtu mmoja kwa mwaka na mwisho wa mwaka wewe na uliyemwelimisha kila momoja atamwelimisha mwingine...nk.
Na kama nusu ya ya watu watakaoelimishwa watajitwika uadilifu). Miongoni mwa watu hawa nitaunda baraza la mawaziri wasiozidi kumi na tano.
Baraza hili likiwa la kizalendo na lenye sifa njema basi ndipo tutashuhudia mambo mengi na sio ajabu wakati huo kuanzisha mipango ya jinsi ya kutengeneza mitambo, mashine mbalimbali, vipelezi vya angani (satelite), utafiti hadi wa kwenda mwezini (lakini yote yatalenga ukombozi wa fikira na utatuzi wa matatizo ya mtz kwanza), nk.
Tunaweza kuifanya tz yetu ikawa nchi inayojiongoza kwa haki na inayoongozwa na utashi mkuu wa kisayansi na tukapita hata mataifa mengi duniani. Maisha ya watu wetu yataboreka, uvivu hautakuwepo, na tutakuwa tumeushinda ujinga, umaskini na maradhi ya akili miongoni mwa watz.
Rasilimali tunazo, watu tunao, uwezo tunao, lazima tujiamini, tutaweza. Niko pamoja nanyi kwa Tanzania yenye baraka. Sina mashaka na nia yangu wala utashi Mungu alioonijalia.
Mungu ibariki nchi yetu.