Hongera sana mkuuHabari za muda huu wana JF,
Naomba kujulishwa kuhusu usafiri wa kutoka DAR mpaka Chuo Cha Ualimu Vikindu,nauli ni kiasi gani na magari yanayoelekea wapi natakiwa kupanda?
Pili,kama kuna mtu anayo joining Instructions ya chuo hicho naomba aiweke hapa screenshot inayoonesha sehemu ya malipo na mahitaji kwa ujumla ili nianze kujiandaa mapema.
Kifaa ninachotumia hakina uwezo wa kufungua PDF files.
Nimechaguliwa kwenda huko kusomea ualimu elimu ya msingi na taarifa imetoka Asubuhi hii.
Asante!
Nadhani maelezo uliyopewa hapo juu yanajitosheleza. Kuna la zaidi? Au pia unataka kuuliza hapo Mbagala utafikaje?
Ok, kutoka Ubungo stendi, sogea mpaka pale river side karibu na Land mark Hostel. Panda gari za Mbagala pale mpaka mwisho. Ukifika pale stendi tafuta gari za kwenda Mkuranga. Panda hizo uwaambie wakushushe Vikindu.
Asante sana!Hongera sana mkuu
Hello wana jf.. Naomba kuelezewa jinsi ya kupata fom ya kujiunga na vikindu teachers college