Naikumbuka Songea enzi, tukumbushane

Naikumbuka Songea enzi, tukumbushane

Private investigator

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
303
Reaction score
287
TV unaenda kuangalia songea club na jumapili ndo disco hapo hapo, ukumbi wa video kwa LUMINA VIDEO SHOW na baadae SHINYANGA VIDEO SHOW. Watoto wa kike toka RUHUWIKO akina Rehema, Shani nk.

Mabitozi akina Aflam. Na ukipendeza lazima jioni ufike ZIMANIMOTO kwenye kikapu. Zikaja chokstik lambalamba, hospital ya veris, mabasi ya Kiswele, OTTAWA alikuwa ana malori manne akinunua kutoka KAURU.
 
Zikaja phonex zakukodi tsh 200 kwa saa. Ukumbi wa shefaz matalawe na lizaboni gest nzuri TOP LIFE kwa Madamba kwa chini.
 
Kuna mkaanga chips mmoja alikuwa kila jioni anauza za mafungu pale msikitini mfaranyaki.
 
Kipindi SAMCO kiwanda cha tumbaku hapo karibu na line za polisi kinafanya kazi, wafanyakazi walitoka kila pembe ya mji, utawatambua kwa harufu zao hata ukikutana nao video show.
 
Yule bwana mapesa aliewahi kuji%&#nyea kwa kugida kwa pupa bia bingwa ni miaka hiyo?
 
songea imetulea uwanja tuliokuwa tunautegemea ni zimanimoto basi watoto kibao wa center tulikuwa tunajaa mle kucheza hadi watoto wa matarawe,mfaranyaki,mabatini,bombambili yani wanafika mechi
 
BOX 2 ndo mitaa yangu, kutembea ni matogoro na chuo cha walimu...., daah for two years. Amazing....
 
Songea girls shule yangu..geti kaaliii unaomba ifike jumapili walau muende kanisani pale Roman Catholic walau mkaangalie mji mnunue karanga na mkate..
 
Back
Top Bottom