fdizzle
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 1,902
- 2,396
Nawasalimia wakuu!!
Mpaka kufikia kuanzisha hii mada naomba nikiri wazi kuwa nimefuatilia kwa kina mijadala unayo endelea kwa sasa hapa nchini.
Nisingependa kuwatoa katika mijadala hiyo lakini pia naomba tuchukue muda kutafakari baadhi ya mambo.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 ulikuwa na changamoto kubwa ya watu kutaka mabadiliko. Naomba nikiri wazi kuwa mimi ni mmojawapo wa waliotaka mabadiliko na kura zangu zote niliwapa UKAWA, na bahati mbaya kura ya rais ndio ilishindwa.
Baadhi ya vitu nilivyotegemea baada ya UKAWA kuchukua jiji ni kufuatilia kwa kina suala la UDA na zile sarakasi za kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani.
Badala yake UDA imewashinda na wamekaa kimya, na cha ajabu zaidi tozo kwa wanaosindikiza wanaosafiri pale ubungo imepanda na cha kusikitisha hakuna uboreshwaji wa miundombinu ndani ya stendi (ukitaka kuijua vizuri kadhia hii nenda wakati wa mvua halafu ukute basi linataka kutoka nawe umechelewa utakanyaga matope bila ya kupenda).
Aliyewahi kuwa waziri mkuu enzi za awamu ya nne ndg. Lowassa alipata kusema bungeni kuwa "anashangaa wananchi wanalalamika na viongozi wanalalamika badala ya kuchukua hatua kutatua kero za wananchi"
Hii kauli naiona inatumika kwa hawa madiwani tuliowapa jiji kwani badala ya kuchukua hatua nao wanalalamika kuhujumiwa sasa sisi wananchi wa kawaida tufanye nini?
Nahuzunika kuona meya akitolea matamko suala la vyeti feki na mbaya zaidi anatoa matamko katika mtindo wa mipasho na tuliowengi wetu tunashangilia na kumsifia.
Nashauri ndugu zangu tujifikirie vizuri haya mambo tunayoshabikia na sio bendera kufuata upepo tu.
Kwa upande wangu najutia kura yangu niliyowapa UKAWA.
Nawasalisha.