Naibu Waziri William ole Nasha amhujumu Rais

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,049
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha, ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotuhumiwa kuihujumu Serikali kwa kuvujisha siri mbalimbali kwa raia wa kigeni.

Tayari kuna taarifa kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimepanga kumhoji juu ya ushirika wake kwa raia wa Sweden anayetajwa kuwa ni ‘jasusi’ kinara wa migogoro katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha.

Kwa siku kadhaa sasa, vyombo hivyo vipo Loliondo, na tayari watu kadhaa wakiwamo wanasiasa, viongozi na wanachama wa asasi zisizo za Serikali (NGOs); wamekamatwa na kuhojiwa.

Pia wamo walimu wawili wa shule za sekondari za Loliondo na Digodigo zilizoko mkoani humo.

Kuhusishwa kwa Nasha kwenye sakata hili kunatokana na taarifa za kiintelejensia zilizowezesha kunaswa kwa mawasiliano yake na jasusi huyo raia wa Sweden, Susanna Nordlund.

Susanna, mwalimu wa lugha ya Kispaniola aliyeacha kazi hiyo na kuamua kukusanya fedha sehemu mbalimbali duniani kwa kigezo cha utetezi wa wafugaji wa Loliondo, anatajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya ujinjifu wa amani kati ya wananchi kwa upande mmoja dhidi ya wawekezaji na Serikali kwa upande wa pili.

Amekuwa akiitukana na kuidhalilisha Serikali ya Tanzania na viongozi wake kupitia mitandao mbalimbali ambayo baadhi anaiendesha na mingine huuza habari. Miongoni mwa mitandao anayoshirikiana nayo ni Avaaz.

Wiki iliyopita, alipopata taarifa za kukamatwa na hatimaye kuachiwa kwa walimu Supuk Maoi wa Shule ya Sekondari Loliondo; na Clinton Kairung wa Sekondari ya Digodigo; aliandika haya kuhusu Serikali: “Great, Now lets hope that those bastards haven’t achieve their objectives”; akimaanisha ‘hawa wanaharamu (Serikali) hawakufanikisha malengo yao.’

Kwa msaada wa NGOs, Susanna aiingia nchini mwaka 2010 akijitambulisha na kupewa viza ya utalii, lakini akatiwa hatiani baada ya kubainika anaendesha mikutano ya uchochezi. Alipigwa faini ya dola 400 za Marekani. Akapewa hati ya kufukuzwa nchini (PI Na. 0039131) iliyotolewa Februari 12, 2010 Arusha.

Mwanzoni mwa mwaka huu, kwa nyakati mbili tofauti ameandika barua Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiomba aondolewe PI, huku akihadaa kuwa yeye ni mtalii. Lakini kazi zake nyingi ambazo baadhi ziko kwenye mitandao ya wazi na mingine ya siri, zinakinzana na ukweli huo.

Hati yake ya kusafiria yenye namba 12011727 aliyoipata Sweden Februari 8, 2001 ikagongwa muhuri kuonesha kuwa hatakiwi kuingia Tanzania.

Aliporejea Sweden akafungua blog ya “View from the Termite Mound”. Huko akajaza makala zinazoendelea kuichafua Tanzania, akitaka kuuaminisha ulimwengu kuwa Serikali inawaonea na kuwaua wananchi (wafugaji) wa Loliondo.

Susanna alibadili hati ya kusafiria na kurejea nchini Tanzania Septemba 2011 kupitia mpaka wa Namanga akitumia hati yenye namba 825 623 97 iliyotolewa Sweden.

Alipitia Namanga akitokea Kenya ambako NGOs nyingi za Ngorongoro, ama zinamilikiwa, au zina ushirikiano mkubwa na Wakenya.

Hapo Namanga alipewa viza ya utalii. Aliingia kwa kutumia hati hiyo na kufikia katika hoteli ya Abba iliyoko Arusha kisha akaenda Loliondo na kuzuru vijiji vya Ololosokwan, Mondorosi, Sukenya, Soitsambu na Kirtalo.

Baada ya hapo akaandika makala nyingi za uchochezi zilizolenga kuwafanya wananchi waichukie Serikali. Alirejea nchini Juni, 2013 kwa kupitia hapo hapo Namanga na kupewa viza ya utalii. Akafikia katika hoteli ile ile ya Abba jijini Arusha kabla ya kuzuru vijiji vya Ololosokwan, Mondorosi, Sukenya na Kirtalo kwa lengo linaloelezwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa ni uchochezi.

Juni 17, mwaka jana akiwa na PI, aliingia nchini kupitia upenyo wake wa Namanga na kupatiwa viza ya utalii! Wawezeshaji wa mpango huo ni NGOs rafiki zake. Alifikia Monjis Guest House, Arusha ambako alikaa kwa siku tatu kisha akaenda Loliondo Juni 20. Loliondo alifikia Oloip Lodge iliyopo Wasso. Juni 23, alikamatwa na kurejeshwa kwao kupitia Kenya.

Hivi karibuni alifika Narok na Porsmoru ambako ni mpakani kwa Tanzania na Kenya; na akawa anafanya mawasiliano na watu wake walioko Tanzania.

Chanzo: Jamhuri
 
Inakuwaje wanashindwa kumkamata? Arusha kuna NGO nyingi sana zinazopata fedha nje kwa ajili ya mgogoro wa Loliondo mojawapo ni PINGO FORUM..Wanawatapeli wazungu kwa kujifanya wanawatetea wamasai
 
mkuu jamaa anaweza amka kesho akakutana na barua kwenye vyombo vya habari
Ikisema utendaji wao hauridhishi
 
Back
Top Bottom