Naibu Meya Dar ni Mussa Kafana, Diwani Kata ya Kiwalani CUF

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,927
244,504
IMG-20160421-WA0054.jpg

Taarifa za vyombo karibu vyote vya habari zimedokeza kuhusu jambo hili .

UKAWA ambao ndio watawala wapya wa jiji hili ikiwa ni rekodi mpya kuwekwa nchi hii tangu Mwenyezi Mungu aumbe mbingu na ardhi , wamemsimamisha Mh Kafana Musa wa CUF .

Kwa vile namba hazijawahi kudanganya basi bila shaka yoyote UKAWA itashinda kwa kishindo.

Kila la heri UKAWA.
=======================

UPDATE

Diwani kata ya Kiwalani (CUF), Mussa Kafana leo achaguliwa kuwa naibu meya jiji la Dar baada kupata kura 10 dhidi ya 6 za Mariam Lulida (CCM)
 
Sasa na Kabwe wameshamtumbua hakuna tena wakufanya kanjanja, jecha asiijue hii issue vingievyo atakuja tengua huo uchaguzi kisha kuitisha mwingine, basi ni lazima tu kumuomba
Mungu asaidie vingimevyo duuuu!!!!
 
Safi sana sasa ni kuchapa kazi iliyotukuka ndani ya miaka hii 5, ilete mafanikio yaliyoshindikana miaka 50.
 
Naibu meya wa jiji la dar es salaam amechaguliwa mchana huu wa leo.hizi ni baadhi ya picha zake baada ya uchaguzi huo

IMG-20160421-WA0054.jpg
IMG-20160421-WA0055.jpg
 
Diwani kata ya Kiwalani (CUF), Mussa Kafana leo achaguliwa kuwa naibu meya jiji la Dar baada kupata kura 10 dhidi ya 6 za Mariam Lulida (CCM)

Hapo hakuna kugawana lawama.Meya na naibu meya wote UKAWA.Wakivurunda zigo lote la kwao.Angekuwa meya UKAWA na Naibu meya CCM hapo kukitokea timbwili au kuvurunda vyama vyote vingebebeshwa zigo na kugawiwa lawama nusu kwa nusu.Lakini sasa Zigo lote la Jiji liko kwenye mabega ya UKAWA.
Kila la heri
 
UKAWA mnasherehekea nini sasa...Nendeni mkafanye kazi...wananchi ndio wataamua kama mnaaminika au la
 
sasa rasmi mgombea wa UKAWA ndiye naibu Meya wa jiji la Dar , kwa faida ya wale wasiofahamu ukubwa wa Naibu Meya wa jiji la Dsm , ni kwamba uwezo wa mtu huyu unafanana na wakuu wa mikoa ya pembezoni kama 10 hivi , hili jiji ndio roho ya nchi yenu , kila kitu nchi hii kinatokana na huruma ya Dsm , wabunge wenu wote wanaishi hapa , mawaziri wa nchi hii wote wako hapa na kubwa kuliko yote ni kwamba hata ikulu ya nchi hii iko hapahapa .
 
Hapo hakuna kugawana lawama.Meya na naibu meya wote UKAWA.Wakivurunda zigo lote la kwao.Angekuwa meya UKAWA na Naibu meya CCM hapo kukitokea timbwili au kuvurunda vyama vyote vingebebeshwa zigo na kugawiwa lawama nusu kwa nusu.Lakini sasa Zigo lote la Jiji liko kwenye mabega ya UKAWA.
Kila la heri

BADO TUMEANZA NA KUIMALIZA CCM MKOANI DSM, KISHA MIKOA YOTE UCHAGUZI UJAO WATAISOMA NAMBA CCM.

BAADAYE TUNAMALIZIA NA KUINGIA IKULU.
 
Back
Top Bottom