nahitaji ushauri wenu wana mmu

Kabla sijachangia naomba kujiridhisha na jinsia yako kwanza @gfsonwin usije ukawa dume jike
 
nisingependa kuzungumzia upande wa dini.....

naomba nikuulize swali ambalo ni out of topic, huyo mwenye mtoto mmoja alikwambia kuwa amemaliza kuzaa?haitaji wa pili? au umejifikiria mwenyewe kuwa unao 3 umeona inatosha? what if akiamua kubeba ujauzito?

nikirudi kwenye mada,hii ni kiubinadamu zaidi(si kidini)
siku zote jamani wanaume msijidanganye kuwa mn uwezo wa kumtosheleza mwanamke..... na siku zote wanaume msifikiri kuna mwanamke anayefurahia kuona anashare 'dushelele' na mwanamke mwenzake....

kama vile ambavyo wewe umeumia ndivyo wake zako kila mmoja kwa wakati wake ndivyo anavyoumia... {mtazamo wangu: hata baadhi ya wanawake wakikwambia 'mume wangu oa dini inaruhusu" ni kuwa amekuruhusu kwa kuwa hana jinsi, mikono yake imefungwa} hivyo hata kama hajatamka wazi mwanamke huyo lazima atatafuta faraja, iwe anapatana au hapatani na mke mwenzie, atattafuta mahala ambako atajiaminisha {hata kwa kujifariji} kuwa yupo mwenyewe.... au atatafuta akiamini kuwa hata wewe unafanya, hata wewe unatoka na una weza kuongeza mke na zaidi na zaidi...


labda nikupe kisa cha mzee mmoja namfahamu.....
mkewe alipata tatizo la uzazi hivyo hakuweza kupata mtoto tena,
pamoja na kuzaa huku na kule na kumletea bi mkubwa watoto akaamua kuoa ilhali dini haimruhusu....
akaoa mke wa pili wakazaa watoto 2...
akaoa mke wa tatu wakazaa mtoto 1
baadae siri ikatoka kuwa mke wa pili ana bwana, ndiye aliyezaa nae hawa watoto 2........kwa lugha nyingine ameuziwa mbuzi kwenye kiroba (point yangu ni kuwa, kumridhisha mwanamke 1 tu ni kazi sembuse hao 3?)

sasa ufanyaje?
  • uzungumze na wake zako kuhusu tabia yao? ingawa sidhani kama itasaidia kumaliza tatizo.... maana watakuja na mbinu mpya...kumbuka kule "nyumba ndogo" ndo wanajazilizia pale palipopungua iwe kimapenzi au kihisia
  • utafute mbinu za kuwaridhisha kimapenzi.....kumbuka kuwa mapenzi sio sex tu, ili umridhishe mwanamke unapaswa uanze nje ya chumba mpaka kitandani....unapaswa uanze toka unavyoamka asubuhi mpaka mnavyoenda kulala usiku, mwanamke anahitaji security, anahitaji ajiamini kuwa huyu ni wangu, ajisikie kupendwa, na ili wake zake watulie na wewe unahitaji kujitoa kwa kila mmoja wao mpaka "aapreciate" kuwa "yes my husband loves me" utawezaje kufanya hivyo hiyo ni homework yako...



na hili ni somo si tu kwako bali hata kwa wale wanaofikiri mkeo akileta nyodo muolee mke wa pili...
chonde chonde jamani hakuna kazi ngumu kama kumridhisha mwanamke....
na kumridhisha mwanamke hakuanzii kitandani.

ohoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

 
Mkuki kwa nguruwe......
Sioni kama kuna tatizo we endelea tu na mapenzi kwa wake zako,kuoa mke mwingine sio solution na hata yy atakua na kidumu tu. Kwaheri

Jamani Yummy hata chembe ya huruma humwonei mtoto wa mwenzio?
 
Na mwanamke kuwa wanaume wawili ndo nini?
 
Lol! nnavyofurahia revenge, wallah nisingechungulia shule ningekuwa mchawi!

Wape salamu wakezo, waambie king'asti wa jf would like to add zem on fesibuku
 
Mkuu gfsowin,hawa dawa yao ndogo,kwa bi mdogo nyumba uza au pangisha and then put them under one roof kisha tuone huo uzanga wataufanyia wapi,pambaf zao.
 
Lol! nnavyofurahia revenge, wallah nisingechungulia shule ningekuwa mchawi!

Wape salamu wakezo, waambie king'asti wa jf would like to add zem on fesibuku

Wanawake mkoje? Mbona mnashabikia maasi? Jamani hizi ni ndoa halali zimebarikiwa na Sheikh,na kama ni kuingia kwenye mitala waliingia kwa hiyari,why should they cheat?gaddammit!
Gfsowin,umeniharibia siku kwa uzi huu.
 
Eiyer mwenzangu sio peke yako....kuna siku huyu mtu alisema amejifungua jamani au mimi ndio nachanganya madawa hapa???

jamani humu jukwaani watu hatuna haja na jisia ya mtu nafikir na wale ambao ni wafuatiliaji wazuri watajua tu mimi ni jisia gani. Anyway mimi ni ke ila nimeandika haya kwani kuna mtu anataka ushauri wa haraka and to be wise nilitaka kuona wengine wangeshauri nini na pia kuwaelimisha wengine. Kwa wale ambao ni psychologist wanajua kwanini navaa uhusika halisi mimi. kwanza ni rahsi kueleweka zaid kuliko kutumia majina au nafsi ya 3.

Pia hiki ni kisa halisi kabisa na nimetoka kutatua jana but mpaka sasa solution haijapatikana shauri li litakaa keshokutwa tena.
 
badili tabia,wapo wake wanaoelewana ila ni wachavhe mno.ninae jamaa yangu mmoja,yeye ni mke wa 2,na mke mkubwa wake wanaelewana mno.kila kitu sare,mpaka watoto wao,wanaelewana sana tu,ilifikia wakati mpaka kitanda wana share na mume wao.sasa hivi wana wajukuu,mpaka hivi sasa wanaelewana.kuhusu topic ya mleta mada.inaonyesha hao wake kuna kitu hakijawaridhisha ndio maana wanafanya hivyo.iliyobaki ukae nao na uwaulize.sometimes kuacha sio kitu kizuri,ila jee wasipobadili tabia upo tayari na wewe ku share?tatizo liko hapo.ila mwanzo waulize,na wawe wakweli kwako.otherwise mtauwana bure kwa huo mzunguko
 
Kwa kuwa wewe una zaidi ya mmoja, sioni tatizo la wao kuwa na mmoja tu. Waache nao wafaidi kile wewe unafaidi kwa kwa kwako na wake wawili.
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
 


Badili Tabia, hili swali ni lamsingi sana katika maisha ya gfsonwin ingawa sidhani kama ndio sababu ya wakeze kutafuta vibuzi.
gfsonwin, uamuzi wa kuwa watoto wanatosha au la yafaa uwe wa pamoja na si wako wewe mwenyewe kama mume. Asikwambie mtu bwana kuzaa kwa mama kuna raha yake na katu si rahisi kumkatili iwapo bado anayo hamu ya kuendelea. Mtoto mmoja kwa bi Mdogo nahisi kama unambania!!


Aksante Badili Tabia. Hili ni somo tosha kabisa ingawa mie naliangalia kwa upande wa pili wa shilingi (pengine ni kwa kuwa siielewi vizuri dini ya wenzangu) Je mwanamke ambaye hayiuko tayari kuolewa mitala anaruhusiwa kukataa? kwa sababu sometimes tunachukulia kuwa wanawake ni viumbe dhaifu ambao hawana jinsi zaidi ya kuyaweka matakwa, mielekeo ya maisha yao kwenye veins za maisha ya wanaume! Hawa kama waliona hawaridhishwi na mume wao si wangemketisha na kumweleza kwanza kabla ya kuichukua hiyo hatua waliochukua??
 
Umejuaje kama wana vidumu
haha watakusuta wake zako
Mwaya Pole sana wakalishe na uwaambie umegundua wanachokifanya kama wataendelea utachukua hatua za kinidhamu
.Ndio maana nikashangaa mke mdogo na mkubwa wanapendana namna hiyo kumbe wana siri sirini
 
Wanawake mkoje? Mbona mnashabikia maasi? Jamani hizi ni ndoa halali zimebarikiwa na Sheikh,na kama ni kuingia kwenye mitala waliingia kwa hiyari,why should they cheat?gaddammit!
Gfsowin,umeniharibia siku kwa uzi huu.

Bishanga sawa kabisa, ndoa ni makubaliano unless hawa wadada walilazimishwa na bado haiwapi justification ya kucheat bwana.
 
asante sana
Yummy ila kumbuka mimi sijaoa kuwakomoa bali
naruhusiwa na wao ni wanawake wanapaswa wawe na mume mmoja tu.

Mmoja tu ambaye anakutimizia mahitaji kila cku sio kila ikifika zamu yako. Wametafuta mtu wa kuku replace wakati haupo nao wakiwa na uhitaji. Acha ubinafsi.
 
Last edited by a moderator:
asante sana Yummy ila kumbuka mimi sijaoa kuwakomoa bali naruhusiwa na wao ni wanawake wanapaswa wawe na mume mmoja tu.

Kwani si tayari wana mume mmoja ambaye ndio wewe mkuu.
Baada ya kusoma bandiko lako nimegundua wakezo hutoka nje kwa kuwa hawapati "full time" ya kukaa nawe.
Tafuta nyumba moja kaa nao wote kwa pamoja maana ushaeleza kuwa wanapatana na kuheshimiana.
Pia hii itasaidia kuwa"monitor" la sivyo mkuu utakuwa unalea dondandugu.
 

Assalaam alaiykum warahmatullah wabaraqatuh! Awali ya yote hongera sana kwa kuifuata aya ipasavyo! Lakini kaka mambo yote yanakwenda kwa mujibu wa Quran na Sunna, hapa ulipokuja kutafuta ushauri kwa maoni yangu sioni kama utapata ushauri stahiki. Mie nakushauri urejee katika Quran na Sunna.
 
Asprin ndio ushauri gani huo????duuuh
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin bora umefunguka nilidhani nimechanganyikiwa,ni vyema ukawa wazi tu ndio utapata ushauri maridhawa.

Kiukweli huyo jamaa asiwaache hao wake zake aendelee nao tu,inawezekana wameshaukwaa.....ukisoma alichoandika Asprin hapo juu inaonyesha jinsi gani kitu itakua inazunguka inasikitisha sana.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…