Nahitaji Ushauri na Mawazo yako

brightondeo

Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
7
Reaction score
2
Habari zenu wana jf,

Mimi ni mgeni humu nimekuja kwenu kuomba ushauri na mawazo yenu, maana humu kuna watu wa rika tofauti na jinsia tofauti. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka kadhaa, nilimaliza elimu ya sekondali miaka michache ilopita, sikufanikiwa kuendelea na elimu zaidi kutokana na familia kutokuwa na uwezo kifedha.

Hivyo ikabidi nikae nyumbani niwasaidie wazazi wangu shuguli yoyote inayohitaji nguvu zangu, baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na shughuli maalumu ya kufanya nilifanikiwa kupata fedha baada ya kucheza upatu. Nilipopata pesa nikapanga kwenda kutafuta maisha mbali na nyumbani, kwa kuwa nilikuwa na rafiki yangu tuliyesoma naye shule aliyekuwa anaishi jijini Dar nilimwambia adhima yangu ya kwenda huko ili nami nikajaribu maisha bila hiyana jamaa alinikubalia.

Nikawaeleza wazazi wangu mpango wangu kwa kuwa sikuwa na kazi yoyote wakanikubalia niende nijaribu riziki yangu, nikaandaa safari kutoka mkoani Mbeya mpaka jijini Dar nikafika jamaa akanipokea vizuri mpaka anapoishi mburahati, nikakaa huku nikitafuta kazi nilipoona sijapata kazi maalumu nikatafuta vibarua vya ujenzi kwenye maghorofa nikapata kwa mchina akawa ananipa 7000 kwa siku nikafanya wiki mbili hali ya hewa ikanikataa nikaumwa bila kutoa taarifa kibaruani nikaaa one week bila kwenda huko kibaruani.

Siku nimeenda nikaambiwa sina kazi maana nimekaa cku nyingi bila kwenda kazini, ikabidi nianze upya kupambana nikitafuta tena kibarua nikaja nikapata kwa Bakhresa MZIZIMA FLOURS MILLS, kazi ya kubeba unga kupakiza kwenye magari na kupanga sehemu husika pale hakukuwa na malipo maalumu na vijana ni wengi yani ubabe na matusi ni kama vile mpo kilabuni unaweza kukuta siku ingine unapewa 4000 siku ingine 7000 yani hapo unakuwa umefanya kuanzia asubuhi saa moja na nusu utapumzika saa saba mpaka saba na nusu.

Baada ya hapo ni kazi kumi na mbili pale machine au mitambo inapozimwa nilifanya kazi siku tano nilinusulika kuvunjika shingo kutokana na jinsi mifuko ya unga inavyotupwa kichwani wakati wa kupeleleka kupandisha kwenye magari, nikaacha nikapata kazi ya ulinzi kwa mshahara wa sh 140000 kwa mwezi yani hakuna kupumzika daily hakuna jumamosi au jumapili hapo nilikuwa nishaingia kupanga chumba changu unalipa 40k kwa mwezi na miezi sita malipo ndo inatakiwa nimefanya ulinzi miezi saba.

Nilipewa taarifa Bibi yangu mzaa baba amefariki kwenda kuomba ruhusa kwenda msibani wakaniambia nikienda huko siku ambazo sitakuwepo hela siesabiwi nikakubali hivyo hivyo nikaenda Mbeya msibani nikakaa siku sita ya saba nikarudi kazini nikaendelea na kazi kama kawaida mwezi wa pili tangu niingie kazini baada ya kutoka kwenye msiba nikaumwa nikapewa siku tatu mapumziko ila niliumwa siku tano kulipoti kazini waniongezee siku wakagoma.

Nikaendelea na kazi hivyo hivyo ikafika siku nikazidiwa kazini kutoa taarifa kwa viongozi wakasema wataleta mtu aje achukue nafasi yangu lkn hakuna mtu aloletwa jioni nikaondoka nikafikia hospital tena nikapewa kitanda siku moja nipo nimelazwa bila kwenda kazini siku nimeripoti nikaambiwa sina kazi nikakaa nikaona sasa nahitaji kujipanga upya maana sikuwa hata na hela ya akiba na kazi sina.

Nikaongea na rafiki yangu akaniambia niishi kwake nikamwambia nahitaji kupumzika akanipa nauli nikarudi mbeya nyumbani nimekaa hapa nyumbani nimeona hali ya hapa cyo nzuri istoshe nilishazaa na mwanamke na mtoto mwenye mwaka na miezi Tisa anahitaji huduma kutoka kwangu nafikilia niludi tena dar nikaanze tena maisha maana chumba changu bado Nina mkataba nacho naombeni mawazo yenu au ushauli je niludi tena dar au nifanyeje ukizingatia nilipo ni kijijini kazi kubwa ni kilimo hakuna kazi zingine.

Karibuni kwa ushauri
 
Mkuu naona unataka kurudi kwenye matatizo yaleyale, nini unaona kitakufanya uishi mjini vizuri endapo utarudi? Hapo mbeya shughuli za kilimo zinalipa acha kupoteza muda wako ukizingatia tiyari una familia inakutegemea
 
Pole kwa yote mkuu
Ila baki mbeya ufanye shughuli za kilimo km ni vibarua utapata huko huko mbeya kwa sasa dar napo pagumu pambana huko ulipo,hiyo nauli ya kwenda dar ifanye mtaji
Jitume sana Utafanikiwa
 
Mkuu naona unataka kurudi kwenye matatizo yaleyale, nini unaona kitakufanya uishi mjini vizuri endapo utarudi? Hapo mbeya shughuli za kilimo zinalipa acha kupoteza muda wako ukizingatia tiyari una familia inakutegemea
Nashukuru kwa mawazo yako
 
Pole kwa yote mkuu
Ila baki mbeya ufanye shughuli za kilimo km ni vibarua utapata huko huko mbeya kwa sasa dar napo pagumu pambana huko ulipo,hiyo nauli ya kwenda dar ifanye mtaji
Jitume sana Utafanikiwa
Asante kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…