kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,335
- 7,744
Wakuu nawasalimu.
Nina tatizo la kukosa furaha, kazini kwangu sina tatizo lolote na mfanyakazi mwenzangu au Maboss wangu.Nalipwa vizuri kiasi maana mshahara wangu net ni zaid ya 1.7,napata incentives nyingine nyingi,nikiwa kazini silipii nyumba.Boss wangu ananijali na kuniheshimu,huwa napata bonuses ambazo hazikuwa kwenye initial agreement mpaka najiona kwa nini sikuja hapa mapema.siku ya birthday yangu nilipewa kiasi cha fedha dola 200 ambazo sikuwa na shida nazo.
Tatizo sina furaha.Asubuhi najilazimisha kuamka kwenda kazini.Mbona ile furaha niliyodhania nikilipwa hivi nitafurahia maisha sina?tangu nije hapa kuna nyumba imefika hatua napaua kwa pesa hizi hizi nazolipwa.Mbona badala ya Furaha nikinyume chake?Najikaza lakini nataka kuiacha hii kazi.Nipo Kaskazini kikazi na nina kibanda kule kwenye magaidi feki.Nahitaji msaada ndugu zangu,natafuta kitu kinachoninyima amani sikioni.Au nimerogwa?Sijui ndio depression yenyewe au ni nini?Naumia nafsi nisaidieni mwenzenu mawazo.Hata kuandika hapa nimeandika tu basi.
Huwa nasoma nyuzi za watu nasema hawa hawana aibu na matatizo yao?mpaka wanaandika humu?lakini naona watu humu wanamatatizo ya aibu wanayaleta mimi hili langu nashindwa kusema?Leo nimewaza nimegundua hili tatizo ni kubwa kuliko navyofikiria.Kila nikilala nasema okay kesho nitakuwa sawa lakini wapi.
Natanguliza shukurani kwa msaada na ushauri wenu.
Wassalam.