Nahitaji msaada

shaks001

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
1,246
Reaction score
1,071
Wakuu,nina elimu ya kidato cha sita.Nina uzoefu wa masuala ya kibenki kwa muda wa miaka 6 sasa,japokuwa nilitoka kazini mwaka jana kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu.

Ninaomba msaada kwenye mambo mawili;la kwanza kama kuna uwezekano wa kupata nafasi ya ajira yoyote ile(halali),hata kama ni tofauti na masuala ya kibenki ili niweze kujiendeleza kielimu wakati naendelea na kazi.

La pili,nina eneo kwa ajili ya kulima,na nimepanga nifanye kilimo cha mbogamboga kama nyanya,vitunguu,matango,matikiti maji n.k.Tatizo hapa ni mtaji wa kuanza kilimo ambao nimefanya utafiti nakugundua inahitajika kiasi cha pesa za kuanzia laki 6 na nusu.

Je,kwa hilo la pili naweza kupata wapi wanapotoa mikopo ya kilimo kwa wanaoanza kilimo?Nitashukuru kwa majibu ya kutia moyo na hata ya kuvunja moyo pia!
 
mkuu hlo la pili ndo zuri ajira ni za tabu isu ni kujiajiri.angalia ktk mabenk wanatoa mikopo na kigezo kimoja wapo ni uwe na mali isiyohamishka kama hyo ulonayo
 
Mkuu pole na matatizo hiyo miaka sita mkuu haukua na wazo la kujiendeleza kielimu hata kupata certificate kaka ya mambo hayo ya kibenki mkuu coz inawezekana ukawa umepata redudance pole sana,kuhusu insu ya mkopo jaribu kucheki na kcb bank kaka wanatoa mkopo kutumia sharia ya kiislamu bila riba nazan hilo shamba litakua dhamana kama upo dar nenda tawi lao la lumumba ndo mahusus kwa hiyo shughuli
 

Kutokana na mazingira niliyoanzia kazi,haikuwa rahisi sana kujiendeleza kwa wakati huo.Nilipangwa sehemu ambayo haikuwa na chuo chochote,na kwa kweli mara nyingi sana tunapokuwa kazini ukishaanza kupokea pesa tunajisahau.Nilipambana nikapata uhamisho kuja jirani na Dar kwa ajili ya kujiendeleza nikakumbana na matatizo mengi sana,kila mwaka nikawa nasogeza mbele.
 
Wapendwa me nadhani posti kama hii ni vema mtu ashauriwe nn cha kufanya,na sio kumlaumu wakat kitu kimeshatokea afanyeje? Daima mtu anapoanguka tusiangalie wapi kaanguka na vp kaanguka,ila cha kuangalia n jins ya kumuinua
 
Hebu nenda nmb au azania bank kajaribu kuulizia..maana najua hawakopeshi kuanzisha biashara..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…