Pole kama kweli uliumizwa. Wasiwasi wangu ni kuwa kwa sasa una 23yrs lakini uliumizwa 7yrs a go, kwa hesabu rahisi ulikuwa chini ya 16yrs je huyo aliye kuumiza alikuwa na miaka mingapi? pia ulikuwa ni uhusiano wa aina gani kwa sababu ulikuwa bado ni mtoto ilitakiwa uwe shuleni. Mimi nadhani ulikuwa ni mtoto na huku stahili kujiingiza kwenye mapenzi bali ulikuwa ni muda wako wa kuwa shule. Kingine achana na mawazo ya mapenzi ya mkataba bado wewe ni binti mdogo unatakiwa utengeneze maisha yako na wanaume watakao kupenda kwa dhati watakuja wenyewe. Kunatofauti kubwa sana kati ya ngono na kupenda, kama shida yako ni ngono basi endelea kama ni kupenda omba mungu na andaa maisha yako then utampata ambaye anakupenda, anakuthamini na ambaye wewe mweyewe utampenda awe wako wa maisha.