Nahitaji meter ya 3 Phase

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Habarini wakuu.

Nina shida na meter ya 3 phase . Kuna watu huvuta umeme kwa ajili ya biashara zao,baadae hubadili matumizi na hivyo kukosa matumizi na meter ya umeme ya 3 phase.

Naomba connection
 
Ukibadili matumizi ya meter Tanesco wanabeba ya zamani ndugu.
 
Swali nje ya mada. Zile wiring za kwenye nyumba kwa ajili ya three phase si zinakua nene ama? Meaning kwamba ukitaka kwenda single phase inabidi ubadilishe na wiring uweke nyembamba for single phase. Yes or no.
 
Swali nje ya mada. Zile wiring za kwenye nyumba kwa ajili ya three phase si zinakua nene ama? Meaning kwamba ukitaka kwenda single phase inabidi ubadilishe na wiring uweke nyembamba for single phase. Yes or no.
Umeme ni mfano wa maji ndugu. kama ukiwa na bomba nene basi una uwezo wa kupitisha kiasi kikubwa cha maji ikiwa msukumo wa maji ni mkubwa.Na kama utakuwa na bomba jembamba basi utapitisha kiasi kidogo cha maji, na endapo msukumo wa maji utakuwa mkubwa basi mabomba yako madogo yatapasuka kwa sababu maji yatakuwa yanafosi kupita kwa wingi kwenye njia nyembamba.

Ukiwa na waya mkubwa basi unauwezo wa kupitisha umeme wowote ule uwe mdogo au mkubwa.
 
Ndugu umenielewesha vizuri sana. Asante sana.

Kwa hiyo kubadisha wiring za nyumba yote hakuepukiki ukihama kutoka 3 to 2 phase?

Au unaweza ukaacha hivo hivo na madhara ni kua umeme utakua mdogooo nyumbani maana sasa "mabomba" makubwa!

Au kibongo bongo watu wanaacha tu hivo hivo.
 

jamaa alishakujibu hapa " Ukiwa na waya mkubwa basi unauwezo wa kupitisha umeme wowote ule uwe mdogo au mkubwa "

japo mimi nna swali kwako, kwanini uhame toka 3 phase, kwenda single,

unless kama 'mzigo' umepungua sanaa kwenye nyumba
 
jamaa lishakujibu hapa " Ukiwa na waya mkubwa basi unauwezo wa kupitisha umeme wowote ule uwe mdogo au mkubwa "

japo mimi nna swali kwako, kwanini uhame toka 3 phase, kwenda single,

unless kama 'mzigo' umepungua sanaa kwenye nyumba
Unajua umeme mkubwa nahisi hata matumizi yake yanakua makubwa kwa nyumba ya kawaida tu. Au sio kweli? Nikisema nyumba ya kawaida namaanisha uko tu na vitu vya kawaida km friji pasi taa na feni. Ondoa kabisa jiko la umeme.
Je bei utakayo unalipa umeme km ukiwa na three phase itakua sawa na three phase mkuu kwa vifaa hivyo hivyo nyumba hiyo hiyo
 
1 phase itakua sawa na three phase mkuu kwa vifaa HIVYO HIVYO

ndio, bei ni ileile

ivi unajua kwanini mtu anaweza 3phase, ni kwakua mzigo wote umekua mkubwa ( umezidi Watts 15000 )

uyu mtu ana pamp za maji 3, friji 4, AC sita, friza 2, taa kibao, jiko la umeme, makorokoro kibao,

sasa ashuke ghafla aweke 1 phase, mita yenyewe ya 1phase haitaweza vumilia, labda jamaa afulie aondoe izo takataka ndani
 
Ooh ok mkuu nimekupata. Kwa mfano huu.
Nimeuliza sababu kuna sehemu nimeweka three phase baasi tu yaani lkn haitakua mzigo kuzidi 15000 Watts. Yaani kawaida sana.
Kwa mimi inamaana hata niende single phase sawa. Hata nibaki three phase sawa coz mzigo wa kawaida sana tena sana.

Ila kwa kua umenihakikishia kua gharama za utumiaji ni mule mule tu baasi umeniaminisha kwamba sina haja ya kurudi single phase niwache tu hiyo three phase.
 
gharama za utumiaji ni mule mule
mita ya 3 phase ni muunganiko wa mita ya 1phase 3, kila moja inasoma kivyake

then inajumlisha readings zote 3 na kutoa reading moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…