Mkuu, inawezekana sana kuanza na 8M au zaidi au pungufu.
Mimi sio muumini mzuri wa kuanza bishara yoyote kwa mtaji mkubwa na wakati wote nikipata fursa ya kushauri huwa nashauri hivyo.
Unapoanza biashara, pesa ni muhimu lakini kuna mambo ni muhimu kuliko pesa na ni mtaji mzuri kuliko pesa.
1.Ujuzi (kwenye biashara husika)
2.Mtandao ulionao kwenye bishara husika.
3.Kiwango chako cha uaminifu
4.Fedha
Unapoanza biashara kwa mtaji mkubwa bila uelewa wa kutosha, ni rahisi sana kupoteza kuliko kufanikiwa.