Mkuu, bima inategemea na uwezo wako, zipo za aina mbalimbali. Jambo la msingi ni kuwa bima ina taratibu zake, mfano NHIF ukishalipia na kupata kadi unaweza kuanza kupata matibabu madogo madogo na vipimo vya magonjwa madogo madogo, ila kama utahitaji kutibiwa magonjwa makubwa mfano matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi na kutakiwa kusafishwa damu kwa mashine, hapa ni lazima ulipie pesa hata kama una bima hadi utakapofikisha michango ya angalau mwaka mmoja.
Bima inaendeshwa kwa kuchangiana, wakati wewe una afya njema au umeugua malaria mara moja tu kwa mwaka, ujue pia mchango wako unamsaidia jamaa mwingine mwenye matatizo ya kiafya makubwa yanayotumia gharama kubwa sana, kwa hiyo ni vizuri uwe na bima ya afya mapema ukiwa na afya njema kabla ya kusubiri upate matatizo ndio uanze kufikiria kujiunga na bima.
Nafikiri utakuwa umenisoma Mkuu.