Nahisi simpendi tena

Nahisi simpendi tena

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
655
Ni binti ambae nimekua nae kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa.Huyu binti nilimpata kipindi anamalizia masomo yake ya chuo kikuu na wakati naingia nae kwenye mahusiano ndio alikua anaingia mwaka wa mwisho wa mahusiano.

Nakumbuka kabla hajamaliza chuo kuna siku tulipishana kidogo kiswahili lakini tuliyaongea yakaisha tukaendelea na mapenzi yetu kama kawaida ingawa ni moja ya ugomvi ambao kila nikikumbuka alivyokua akinitreat najikuta namchukia sana ingawa simwambii kwamba kumbukumbu ya ule ugomvi wetu mpaka leo haijafutika kichwani mwangu.

Kuna wakati nawaza kubadilisha laini yangu ya simu ili tu asinipate hewani kwa kipindi hata cha miezi miwili lakini huruma inanijia kwamba atahisi huenda nimeona amemaliza chuo na kuwa mzigo kwangu ndio maana nataka kumuacha.

Nikikumbuka alivyokua akiniletea dharau wakati namtafuta ili tuyaongee kipindi kile tumegombana nashikwa na hasira zaidi ingawa yeye mwenyewe simwambii.

Nifanyeje ili niondokane na hali hii ?
 
Kitu cha kufanya ni kuzungumza nae aelewe hisia zako, mkiweza kuelewana vzr bas mtayamilza ila mkishindwa kuelewana kila mtu aendelee na maisha.
 
Alikufanyaje? Kwa nini usikamilishe simulizi yako tujue na upande wake ilikuaje.
 
Kama ulimsamehe ila bado ukikumbuka dharau alizokufanyia bado unaumia sio suala dogo...binadamu huwa tunasamehe kweli ila ile kumbukumbu ya tukio mara nyingi huwa inabaki

Umekiri kuwa mapenzi yameisha kwake...ninavyojua mie mtu akishafikia hatua ya kukosa mapenzi kwa mpenzi wake means hakuna tena mapenzi

Mie nakushauri uachane nae japo sio jambo zuri kushauri hivyo ila ndio solution iliyopo kwa upande wako...huruma lazima iwepo kwasababu ni mtu uliyedumu nae kwa muda mrefu

Weka huruma pembeni,muache mapema ili yasifike mbali zaidi akaja kukulaumu badae umempotezea muda wake

Kuacha/kuachwa ni kawaida sana katika mahusiano
 
Asante kwa ushauri
 
Hujajua maana ya kusamehe na inaonekana ameanza kupoteza mvuto kutokana na umri. Fanya unaloona linafaa kwa umri wako, ungekuwa mtu mzima kama sisi ungekuwa usingefika huku.
Fafanua kidogo hiyo falsafa ya kupoteza mvuto
 
Mmmnh...Usimpotezee binti wa watu muda. Muache aende zake atapata wa kumpenda..
 
Fafanua kidogo hiyo falsafa ya kupoteza mvuto
Namaanisha kuwa kwasasa hata ukiwa nae hisia zinakuwa low au normal tofauti na mwanzo. Vile vile mwanamke akikomaa upo nae kwenye ndoa ni rahisi kumvumilia kuliko anaekomaa mkiwa separate. Hivyo hakuvutii kiivyo na ukichanganya na vijitabia fulani ndo unakata stim kabisa.
 
ushapata demu mwingine wewe......hapa unataka kuhalalisha.....mwache aendelee na maisha yake....
 
Muafaka ni kumueleza ukweli ili kila mmoja awe na maamuzi yake.
 
Ni binti ambae nimekua nae kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa.Huyu binti nilimpata kipindi anamalizia masomo yake ya chuo kikuu na wakati naingia nae kwenye mahusiano ndio alikua anaingia mwaka wa mwisho wa mahusiano.

Nakumbuka kabla hajamaliza chuo kuna siku tulipishana kidogo kiswahili lakini tuliyaongea yakaisha tukaendelea na mapenzi yetu kama kawaida ingawa ni moja ya ugomvi ambao kila nikikumbuka alivyokua akinitreat najikuta namchukia sana ingawa simwambii kwamba kumbukumbu ya ule ugomvi wetu mpaka leo haijafutika kichwani mwangu.

Kuna wakati nawaza kubadilisha laini yangu ya simu ili tu asinipate hewani kwa kipindi hata cha miezi miwili lakini huruma inanijia kwamba atahisi huenda nimeona amemaliza chuo na kuwa mzigo kwangu ndio maana nataka kumuacha.

Nikikumbuka alivyokua akiniletea dharau wakati namtafuta ili tuyaongee kipindi kile tumegombana nashikwa na hasira zaidi ingawa yeye mwenyewe simwambii.

Nifanyeje ili niondokane na hali hii ?
Fanya kile moyo wako unataka jipe amani ya moyo kwanza kama humpendi mwache
 
Back
Top Bottom