Nafasi zote za madaraka kushikiliwa na makada

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
843
Kuna kila dalili kuwa kuna maamzi yamefikiwa ya kuhakikisha vyeo vyote vya madaraka vinaenda kukabidhiwa makada watiifu ili waweze kusaidia juhudi zilizo kusudiwa za kufikia malengo yaliyokusudiwa mapema iwezekanavyo!.

Dalili zinaonyesha kuwa kwa sasa kuna ugumu wa kwenda kwa kasi inayotakiwa kwa sababu kumekuwa na mchanganyiko wa viongozi ambao siyo makada, hivyo wengi wao wanaweza kukwamisha jitihada kwa makusudi, ama kwa kutumiwa na watu wasiopendelea uongozi uliopo!,

Zaidi ya yote ni dhahiri kuwa sasa tunakoelekea chama kinaenda kushika hatamu!. Hebu nisubiri nione dalili hizo kama zinaweza kuleta uhalisia huo!.
 
Chama kimoja kinarudi kwa kasi nafasi za utumishi wa umma zinashikwa na makada wa chama tawala sio sawa kabisa! Lengo ni kuua upinzanji au! Hivi DED aliekosa ubunge anapewa u DED atatangaza matokeo ya ushindi kwa wapinzani?
 
Hilo ndilo linalohitajika kwa sasa!.
 
Kuna kila dalili kuwa kuna maamzi yamefikiwa ya kuhakikisha vyeo vyote vya madaraka vinaenda kukabidhiwa makada watiifu ili waweze kusaidia juhudi zilizo kusudiwa za kufikia malengo yaliyokusudiwa mapema iwezekanavyo!. Dalili zinaonyesha kuwa kwa sasa kuna ugumu wa kwenda kwa kasi inayotakiwa kwa sababu kumekuwa na mchanganyiko wa viongozi ambao siyo makada, hivyo wengi wao wanaweza kukwamisha jitihada kwa makusudi, ama kwa kutumiwa na watu wasiopendelea uongozi uliopo!, zaidi ya yote ni dhahiri kuwa sasa tunakoelekea chama kinaenda kushika hatamu!. Hebu nisubiri nione dalili hizo kama zinaweza kuleta uhalisia huo!.

Civil servants nao watakuwa makada
 
Kwwkweli haijulikani nini lengo hasa kama ndivyo italeta migogoro kazini kwa baadae make sasa hivi maofisini kutakuwa porojo za kisiasa tu
 
kwa sasa huko tunakokwenda mkuu wa chuo, mganga mkuu, mkuu wa shule nk lazima uwe ni kada kindakindaki.....katiba yetu inaendelea kusiginwa kwa kasi.
 
Hehehe mmeanza kujisomesha namba wenyewe, katiba so inamruhusu au, na hii nayo mtasema ni dikteta mlitaka ateuwe wacongo au wafilipino
 
siku zote wenye akili hujifunza kutokana na makosa maana tulikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja mambo mengi yalikwama na hakuna mtu aliye hoji na mashirika ya umma yaliongozwa kwa itikadi ya chama na yote ya kafa je kweli mfumo wa chama kumoja unatija kwa nyakati hizi?
 
Chama kimoja kinarudi kwa kasi nafasi za utumishi wa umma zinashikwa na makada wa chama tawala sio sawa kabisa! Lengo ni kuua upinzanji au! Hivi DED aliekosa ubunge anapewa u DED atatangaza matokeo ya ushindi kwa wapinzani?
Hata kabla hujaenda kwa wapinzani-fikiria mtu aliye gombea au aliyejaribu kugombea ubunge kwa chama fulani tayari amesha onyesha upande anaolalia. Ukimpa huyu uDED atachukua nafasi hiyo kujitayarisha kwa uchaguzi ujao pamoja na kutaka achaguliwe na chama chake-meaning kazi yake itakuwa na ukada ndani. Sijui huyu atasaidia halimashauri yake vipi kwani akili yake itakuwa kwenye ubunge. Pili sidhani kama atakuwa neutral kwenye kutoa huduma. Hawa wangefaa zaidi uDC.
Kingine ninachoona hapa kuna mtego unaowekwa kuonyesha kuwa ukiwa msomi ukawa mwanachama wa kile chama chetu inalipa-hii ni incentive ya kuvutia wasomi zaidi kwenda chama hicho lakini inaweza kupunguza morali ya carrier civil servants kwani ukifanya kazi chini ya DED-Mwanasiasa lazima kutakuwa na madhara yake.
Nafikiri tutenganishe kazi za kisiasa na za civil servants na kila moja iwe na mkondo wake. Haifurahishi kuona DED "hati anapandishwa cheo" nakuwa DC. Sasa huyu kama anavuliwa uDC ina maana anaweza kurudi kuwa civil servant tena? Naona kuna tatizo mahali sijui watu wa PSPA wanalionaje hili (tuache kwanza sheria inasemaje).
 
Moja ya kitu kilichomfanya Warioba kuchukiwa na kutukanwa sana na ccm ni lile jaribio lao la kuondoa mfumo wa chama dola. Na walifanya hili kwa kujaribu kutenganisha mihimili wa serikali na bunge. Mfano mawaziri kutokuwa wabunge. Kuondoa nafasi za kisiasa km ukuu wa mkoa na wilaya. Na kumpunguzia rais madaraka hasa ya uteuzi! Hili jambo liliitisha sana ccm na wakalitupilia mbali mapema sana! Sasa naona chama dola kinasimikwa kwa nguvu zote huku ikijulikana kwamba huu mfumo umepingwa sana na wananchi!
 
Hili unalolisema ingewezekana basi nchi yetu ingeingia ukurasa mwingine, sasa haikuwezekana tuendelee kuishi kulingana na mifumo iliyopo!.
 
Nimeshachukua kadi ya CCM nimechoka kuisoma namba natega nafasi za kazi mana utumishi hawana issue tena kazi zinatoka CCM
 
Kampeni za 2020 zinaanza. Chama tawala wanajua kua watanzania wengi hawana imani nao tena. Inawezekana wanatumia mfumo huu kurudisha imani kwa wananchi kutokana na utendaji wao. Tutaona itakavyokua.
 
Back
Top Bottom