Nafasi za kazi Platinum Credit

Nafasi za kazi Platinum Credit

Lexus SUV

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2016
Posts
5,131
Reaction score
6,368
Kizuri share na wenzio Bongolanders

====
TANGAZO LA NAFASI ZA PLATINUM CREDIT LTD

Job Title: Wakala wa Mauzo
Location: Dar es salaam
Platinum Credit Ltd
Job Summary
Platinum Credit Ltd inatafuta Wakala wa Mauzo kwa haraka
- Minimum Qualification:Unspecified
- Experience Level:Mid level
- Experience Length:No Experience/Less than 1 year

Majukumu
a) Kupanga sehemu ya kwenda kufanya mauzo
b) Kushiriki katika shughuli za masoko na kutangazabidhaa za kampuni
c) Kujibu maswali ya wateja
d) Kumuelekeza mteja kujaza fomu pamoja na nyaraka zinazohitajika

Sifa za muombaji
a) Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea
b) Awe na uzoefu wa kazi za mauzo na masoko
c) Awe na uwezo wa kujieleza
d) Awe na utayari na uwezo wa kujifunza kazi kwa haraka
e) Awe na smartphone
f) Awe na umri wa miaka 20–27
g) Awe anaishi Dar es Salaam

Jinsi ya kutuma maombi
Muombaji anatakiwa kutuma barua ya maombi iambatane na wasifu wa kazi (CV) kwa barua pepe careerlbf@platinumcredit.co.tz kabla ya tarehe 02/11/2019.
 
Attachments

Jamani uafisa mikopo ni kazi ya stress mno jamani niliisha mwili mimi watu wanachukua mipunga hawalipi. wanaofahamu nikiongea kitu inaitwa portfolio at risk wanaelewa walowahi fanya credit/loan officers. Ila niwatakie kila la kheri
 
Elezea vizuri hapa
 
Ni hivi kazi ya Mkopo. Kutoa,kukusanya,kufuatilia yan monitoring&dispach,collection,follow up. Na hii kazi unakuwa na list yako ya clients ulowapa mkopo na target inategemeana na kampuni ila kwa kawaida clients sio chini ya 300 na uwamanage wakitoka sita waingie sita. Unaeza kuta portfolio yako dispatch 70milioni credit..hivi inabidi udai izo zirudi na interest tena kwa wakati ucheze na portfolio per usipotimiza target hii kazi unafkiri unafukuzwa unajiondokea mwenyewe kwa aibu. Kwenye kutoa sio kazi sababu by nature kila mtu anataka ela shughuli kwenye collection sasa usiombe wateja wakukimbie unapigiwa simu mpaka saa 4za usiku. Ukishtuka usingizini kitu cha kwanza unaona portfolio. Hii kazi sio ya offcn mazee jua lako mvua yako. Inahitaji uwe strong enough
 
platium watanzania wamegoma hawatak kaz au maan kila siku mnatangaza tu
 
Hao jamaa kwa mwezi wanalipa kiasi gani?
 
kazi ya uafisa mikopo ni changamoto sana..niliwahi kufanya kwenye microfinance flani kama intern..asee niliomba poo mwenyewe.
 
hii kazi haina tofauti na kuchunga ng'ombe kijijin sema mjin uku unachunga watu sio ng'ombe
 
Back
Top Bottom