Nafasi ya kazi

Endeleaaa

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,485
738
Tunahitaji mtu wenye uwezo wa kufanya sales:

Sifa:
1. awe ana uwezo wa ushawishi kwa wateja wapya kununua vitu tunavyouza
2. awe tayari kusafiri nje ya Dar es salaam kila itapohitajika kufanya hivyo
3. awe mtu wa kuweza kujisimamia mwenyewe na malengo atakayowekewa kimauzo
4. Afahamu kuongea Kiswahili na Kiingereza
5. awe na uwezo wa kutumia Kompyuta
6. Uzoefu wa kazi wa miaka miwili au zaidi

Tuma barua yako na CV kwa email: info@diginettz.com

Managing Director
Diginet Enterprises
P.O.Box 62062
Dar Es Salaam
 
best thanx a lot for the information.they didn tell us who are most requred, how about degree holder
 
Wewe Murra wa marwa si nimesikia kule kwenu kuna ajila ya kulima bangi, sasa hizi ajila za huku mjini unazitafuta nini moghaka? taitakya tata.
 
Wewe Murra wa marwa si nimesikia kule kwenu kuna ajila ya kulima bangi, sasa hizi ajila za huku mjini unazitafuta nini moghaka? taitakya tata.

Wacha tata!

hata ukirima bangi hakuna barabara kwa hiyo hata kuisafirisha ni shida. Pale mpakani hadi uwe na kitu kidogo cha kuwapatia ware maafande wa doria, mmh imenishinda.
Basi nikaamua kuja hapa mjini nimefanya biashara ya mayai, nimeishia kupata hasara na kukata mtaji baada ya baskeri yangu kugongwa na magari nikiwa barabarani, si unajua barabara zetu nyingi hakuna sehemu maarum ya wapita njia na waendesha baskeri. Na wenye bajaj siku hizi nao wamekuja juu kwa kuvunja sheria za barabarani. Kutoka gongo la mboto hadi sinza siyo umbari mdogo kwa kusafirisha mayai kwa baskeri.
Sijakata tamaa ya maisha murra, natafuta ajira nyingine maana warianiidi ajira ya uporisi rakini na nayo irihitaji kwanza nitoe kitu kidogo....Tanzania ni ya wenyewe murra.
 
Murra, kama unaweza kuna ajira hapa Gema, ulinzi itakufaa? mshahara mtaelewana, lakini umepitia mgambo tata? kisha kuhusu biashara ya mayai mbona inalipa sana?
 
Murra, kama unaweza kuna ajira hapa Gema, ulinzi itakufaa? mshahara mtaelewana, lakini umepitia mgambo tata? kisha kuhusu biashara ya mayai mbona inalipa sana?

Wacha tata murra, siku hizi hata luga ya kikurya kinanitoka
mayai yanaripa sana lakini tatizo ni accident barabarani kwani inabidi niendeshe wakati mwingine sambamba na magari na madereva wa daladara walivyo hawana adabu basi huishi kupigwa pasi na kuanguka mayai yakivunjika na mikosi kama hii ikitokea mara 2 basi tena mtaji unakuwa umeshakufa. GEMA nilishafanya kazi wakanifukuza eti nimedai nyongeza ya mshahara kwa vile nilipiga doble shif siku nne mfururizo. Acha tu tu
 
Hi you have to consider people who have no experience, like i .... i have just completed my secretarial course and i can use computer also i can do any job and i know how to deal with customers......... is it that we college level we will not get vacancy for working if you need only experience one.
(selihope200@yahoo.cco.uk)
 
Murra wa Marwa,

Tata, pole sama haya yote ni maisha, ila tata kuna kale kakazi ketu murra, kule jeshini unasemaje kwa hilo, je una kaelimu ka kidatu cha 4 au 6? kana una elimu hiyo basi kale kakazi ketu(jeshi) kanapatikana june, na je vipi kakifua kako ni kazima?
 
Tunahitaji mtu wenye uwezo wa kufanya sales:

Sifa:
1. awe ana uwezo wa ushawishi kwa wateja wapya kununua vitu tunavyouza
2. awe tayari kusafiri nje ya Dar es salaam kila itapohitajika kufanya hivyo
3. awe mtu wa kuweza kujisimamia mwenyewe na malengo atakayowekewa kimauzo
4. Afahamu kuongea Kiswahili na Kiingereza
5. awe na uwezo wa kutumia Kompyuta
6. Uzoefu wa kazi wa miaka miwili au zaidi

Tuma barua yako na CV kwa email: info@diginettz.com

Managing Director
Diginet Enterprises
P.O.Box 62062
Dar Es Salaam

kwa yeyote anayetaka maelezo zaidi asione uvivu kuandika email kwa hiyo address hapo atajibiwa vizuri. Kama malipo yao hayaridhishi si lazima uchue hiyo kazi. unaoona kidogo kwako mwingine kwake ni zaidi ya kikubwa
 
Nafasi ya kazi zaidi:

Ku install Dish za TV

Kwa yeyote anataka kazi. malizo ni kwa kulingana na kazi uliofanya.

tuma maombi yako kwa address hiyo hapo juu.

kumbuka kazi ya sales bado ipo na mkataba wake ni mzuri sana
 
Mimi natafuta kazi hapahapa Arusha kwenye kitengo cha account. Nina experience ya miaka nane sasa. Nina uwezo mkubwa wa kuongoza department ya accounts. Iam a dynamic mgr. call 0753109803
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa habari njema lakini ninaomba unieleweshe ni mtu wa aina gani anahitajika yaani professional na reference kutoka wapi?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom