Nafasi 20 za kazi

Nafasi 20 za kazi

Comi

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
3,328
Reaction score
958
NAFASI ZA KAZI

SmartMoney inatoa huduma za kifedha bure bila malipo katika akaunti za akiba za simu na huduma za malipo. Kampuni ilianzishwa mwaka 2010 na mwekezaji wa Marekani aitwaye Michael Spencer.SmartMoney Tanzania inamilikiwa na kusimamiwa na wawekezaji wa Marekani na Tanzania na kuendeshwa na wafanyakazi wa Tanzania mjini Mwanza na Kishapu yenye leseni na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania. Ofisi zake zipo maeneo yafuatayo: Kishapu - Mhunze Road, P. O. Box 505 Shinyanga, na Liberty Street ,Mwanza.

Kunahitajika vijana wakujaza nafasi 25 kwa wenye sifa:

Majukumu:
1. Kuwapa motisha na faida ya SmartMoney wakulima, wanakijiji
2. Kutoa elimu kwa wenye maduka.
3. Kujiandikisha wakulima, wanakijiji na wenye maduka kwa ajili ya kujiunga na kufungua akaunti ya SmartMoney

MSHAHARA:
185,000 / = kwa kila mwisho wa mwezi.
100,000 /= nyongeza kulingana na mauzo ya mfanyakazi kwa kila mwisho wa mwezi. 3,000 / = ya chakula kila siku uwapo kazini.

Mbali na hayo kampuni itatoa vitu vifuatavyo:
1. Usafiri wa kwenda eneo la kazi ni pikipiki ya kampuni pamoja.
2. Fulana (Tshirt) ya SmartMoney
3. Kitambulisho cha mfanyakazi.

MAMBO AMBAYO MWOMBAJI ANATAKIWA KUZINGATIA:
Mwombaji anatakiwa kujua matumizi ya digital camera au kamera ya simu ambacho Anatakiwa kuja na kifaa chake mwenyewe ambacho kinaruhusu memory kadi kwa ajili ya kumbukumbu zake.

Muda wa kazi ni siku sita za wiki na baadhi jumapili kulingana na watakavyopangiwa. Kazi inaanza saa 3 asubuhi hado saa 11 jioni.

Kwa wafanyakazi wa muda(PART-TIME SALES PERSON) vipengele vitakuwa kama vya waajiriwa isipokuwa watakuwa huru kufanya shughuli zao zingine. Watalipwa kulingana na utendaji wao wa kazi katika maeneo yao.

Maombi yatumwe kupitia SmartMoney Tanzania P.O. Box 505 SHINYANGA au maeneo yafuatayo
Mhunze – ofisi ya SmartMoney, Shinyanga mjini- Radio Faraja au metika stationery opp. CRDB Bank.
Ikonda- Shija Maige, Idisa- Esta Daud, Mwigumbi-Emmanuel Jiddah, Bunambiyu- Emmanuel Tagala, Buchambi- Leah Peter,Masanga- John Shagembe, Mwalata- Benjamini Juba,Isemelo Chiluli, Isagala- Kepha Masengwa, Ngofila- Hosea Mhoja,Malwilo Msafiri Kasoga,Mwamashele – Laurent Stephano,Ndololeji –Lugesha, Ukenyenge- kwa Mwalimu Hemed.
au kupitia inquiries@smartmoneyproject.org

Waweza kuwasiliana nasi kupitia simu namba 0782004226 au 0769224909

MAOMBI YATUMWE KABLA YA TAREHE 18/01/2015
 
Mnataka vijana wa elimu gani?

nadhani ni kuanzia form four sina uhakika sana ila namba zao za simu ziko hapo nimechukua tangazo kama lilivyo
 
Sasa kama me nikituma barua y Maombi itafka lini na muda unakalibia kuisha wa kupkea maombi
 
acheni uhun wenu, tumejiajiri.

mmejiajiri wangapi? walimu, tra na makampuni mengine wanaodai mishahara wanajidai mishahara au? acha dharau. kama umeshiba ni wewe. wako wenye kuhitaji angalau kibarua na hawapati. hizo ni tabia za ubinafsi
 
Back
Top Bottom