Naenda kuumbuka ukweni, utoto wa mjini umeniponza

appoh

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
5,194
2,110
Leo kutakua na kikao na sherehe ukweni, mimi ni mnyamwezi wife ni mnyamwezi.

Tatizo lipo kwangu lugha haipandi na kama unanyojua wanyamwezi wakikutana wanavyopenda kuongea lugha sijui nitakua mgeni wa nani sikua na muda na mambo ya kikabila kabisa kipindi nakua.

Shija, Masanja, Mabula, Ngosha nisaidieni ushauri nini cha kufanya kujiokoa.
 
leo kutakua na kikao na sherehe ukweni
mimi ni mnyamwez wife ni mnyamwezi tatizo lipo kwangu language haipandi na kama unanyojua wanyamwezi wakikutana wanavyopenda kuongea language sijui ntakua mgeni wa nani
sikua na time na mambo ya kikabila kabisa kipindi nakua

shija .masanja.mabula.ngosha. nisaidieni ushaur nn cha kufanya kujiokoa
mkuu.., Wee ongea lugha ya shemeji zao "kiaarabu" !!! watakusikia
 
Weka udhuru babaa alafu tuma muwakilishi lakini awe rafiki yako wa karibu
 
Nenda na Dirtionary ya Nyamqezi to Swahili yani utakuwa unacheza na page tuu...
 
Usiogope, huendi kuoa ukoo wala kabila wala nyumba nzima. Kule unaenda kunyakua mmoja tu ambaye kishakuzimia fegi. Mfunge kamba binti aijekutupa akifika kwao. Kama anakukubali weye sasa nenda kiuhakika utamrudisha darisalama salama salimini. Unadanganywa ati umpeleke mkalimani, hao hawakutakii mema. Ka weye ni miye ningemwambia my wife to be anitafsiriye yeye na si mwingine. Wengine wote wenge tu
 
Mimi nikifika goweko nikisemeshwa najibu kiswahili likinipita nafanya kuitika abeee, abeee mwisho wenyewe wanarudi kwenye lugha ya Taifa vinginevyo anapatikana mkalimani pale pale, fanya hivyo mkuu, leta mrejesho
 
Back
Top Bottom