Crystal field theory
JF-Expert Member
- Sep 16, 2014
- 951
- 412
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
KUONGEZWA KWA MUDA WA
KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA
CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA
WA MASOMO 2016/2017
Date Posted: 8th August 2016
14:46:59 Posted By: NACTE
Baraza linapenda kuwaarifu wote
walioomba kudahiliwa katika kozi za
cheti na diploma na umma kwa
ujumla kuwa muda wa nyongeza wa
kutuma maombi kwa mwaka
2016/2017 umeongezwa hadi tarehe
13 Agosti 2016 ili kuruhusu ambao
hawakukamilisha maombi yao
kuyamaliza na ambao hawajafanikiwa
kuomba kutuma maombi yao.
Baraza linaomba ifahamike kuwa
vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana
tena wakati wa maombi bali kozi
zitakazoonekana ni zile zenye nafasi
tu pia baraza linashauri waombaji
wajipime na kuangali ushindani wa
kozi ili kufanikisha kuchaguliwa
kwao. Vyuo na kozi zilizo na nafasi
zimeainishwa hapa .
Baraza pia linapenda kuwaarifu
waombaji waliofanya maombi kwenye
vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa
uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri
mwongozo wa Serikali na hivyo
watafahamishwa punde uteuzi
utakapokamilika. Waombaji wa vyuo
hivi wanashauriwa kusubiri na
kutokubadili machaguo yao hadi
kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya
Ualimu vya Serikali.
Baraza pia linapenda kuwataarifu
waombaji waliokwisha chaguliwa
kwenye awamu ya kwanza na
wanataka kuomba uhamisho kutoka
kozi ama chuo kimoja kwenda
kingine wavute subira utaratibu
utatolewa mara tu majibu ya
waombaji wa awamu ya pili
yatakapotolewa.
Aidha Baraza linapenda
kuwafahamisha waombaji wa
Shahada ya Kwanza ( Bachelor
Degree) waliofanya maombi kupitia
mfumo wa pamoja wa udahili wa
Baraza kuwa utaratibu wa
kukamilisha maombi yao utatolewa
baada ya mashauriano kati ya Baraza
na Tume ya Vyuo Vikuu
yatakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 08th Agosti, 2016
KUONGEZWA KWA MUDA WA
KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA
CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA
WA MASOMO 2016/2017
Date Posted: 8th August 2016
14:46:59 Posted By: NACTE
Baraza linapenda kuwaarifu wote
walioomba kudahiliwa katika kozi za
cheti na diploma na umma kwa
ujumla kuwa muda wa nyongeza wa
kutuma maombi kwa mwaka
2016/2017 umeongezwa hadi tarehe
13 Agosti 2016 ili kuruhusu ambao
hawakukamilisha maombi yao
kuyamaliza na ambao hawajafanikiwa
kuomba kutuma maombi yao.
Baraza linaomba ifahamike kuwa
vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana
tena wakati wa maombi bali kozi
zitakazoonekana ni zile zenye nafasi
tu pia baraza linashauri waombaji
wajipime na kuangali ushindani wa
kozi ili kufanikisha kuchaguliwa
kwao. Vyuo na kozi zilizo na nafasi
zimeainishwa hapa .
Baraza pia linapenda kuwaarifu
waombaji waliofanya maombi kwenye
vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa
uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri
mwongozo wa Serikali na hivyo
watafahamishwa punde uteuzi
utakapokamilika. Waombaji wa vyuo
hivi wanashauriwa kusubiri na
kutokubadili machaguo yao hadi
kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya
Ualimu vya Serikali.
Baraza pia linapenda kuwataarifu
waombaji waliokwisha chaguliwa
kwenye awamu ya kwanza na
wanataka kuomba uhamisho kutoka
kozi ama chuo kimoja kwenda
kingine wavute subira utaratibu
utatolewa mara tu majibu ya
waombaji wa awamu ya pili
yatakapotolewa.
Aidha Baraza linapenda
kuwafahamisha waombaji wa
Shahada ya Kwanza ( Bachelor
Degree) waliofanya maombi kupitia
mfumo wa pamoja wa udahili wa
Baraza kuwa utaratibu wa
kukamilisha maombi yao utatolewa
baada ya mashauriano kati ya Baraza
na Tume ya Vyuo Vikuu
yatakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 08th Agosti, 2016