NACTE taarifa kwa uma

KingDenis

Senior Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
197
Reaction score
93
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Date Posted: 2nd September 2016 17:20:21
Posted By:
NACTE

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016.

Baraza pia linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.

Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.


Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 02 September, 2016
 
Nacte hawaelewek chuo kama ATC kimeshachukua watu wake na wameanza masomo lkn vyuo vngne bado na nacte hawaelewek
 
Duuuh
 
NACTE wanawachanganya wananchi.hiyo orodha ya awamu ya kwanza waliochaguliwa majina yako yako wapi? huu mtindo wa kuwachanganya wananchi sio sawa.kuna watu waliomba nacte toka May lakini mpaka leo kimya kwa nini majina ya walio chaguliwa wasipelekwe kwenye vyuo husika?
 

Hapo ndo nimemaliza application sasa iv swal jr nitaweza kutoka katika majina ya awal ya walioapply mwisho agosti 31 au itakuwaje ?
ila registration nilifanya kabla ya agust 31
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…