Muwindaji
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 245
- 206
Habarini wanajamvi!
Waswahili wana kamsemo kao wanasema, Ukiwa Muongo, usiwe msahaulifu!
Edward Ngoyai Lowassa ni mmoja kati ya wanasiasa wazoefu, na wenye kipawa kikubwa cha ushawishi na ukongwe wa kujua kila baya linalotokea ndani ya siasa za nchi hii.
Watu wa karibu wa bwana Edward Lowassa waliwahi kuthibitisha miaka kadhaa ya nyuma kuhusu kile kinachoitwa "Mfadhaiko Mkubwa" alioupata Edward Lowassa baada ya kashfa ya Richmond, iliyomfanya ajiuzuli uwaziri mkuu, kutokana na shinikizo la wapinzani(Ambao walikua ni Chadema kwa sehemu kubwa).
Kwasababu Lowassa alikua ni mwanasiasa mwenye kila kitu, pesa, ushawishi, uzoefu Skendo hii inaonekana ndio iliyokuja kuweka "gundu" kwenye ile ndoto yake ya muda mrefu sana ya siku moja awe raisi wa Tanzania.
Ni dhahiri kwamba EL alijenga chuki kubwa na watu waliohusika kutaka kuififisha ndoto yake ya kisiasa. Chuki hii ilijidhirisha baada ya kuwepo kwa matukio kadhaa ya sintofahamu juu ya watu walioiharakatia kashfa hii, akiwemo aliyekua mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi wa sakata hili kuugua ugnjwa wa ajabu baada ya kusemekana kwamba aliwekewa sumu.
Hali hii ikasababisha, ndugu EL asimame kama nembo ya ufisadi Tanzania, hata baadhi ya wasanii walishatumia jina lake kumaanisha hivyo. Akiwemo Roma Mkatoliki ambaye aliimba kwenye nyimbo yake moja hivi kwamba "Nakomba pesa zote natambaa kama Lowassa"!
Kama kuna jambo ambalo lilikua linamnyima usingizi Lowassa ni kwamba, atajisafisha vipi kwenye huu ulimwengu wa uwepo wa mitandao ya kijamii na jamii inayopata taarifa kwa wakati? Yaani kwa kifupi ni kwamba mpaka mwaka 2010 tayari taifa lote lilikua linajua kwamba Lowassa ndio Muhusika mkuu wa sakata la Richmond!
Lowassa alikua anatambua fika mifumo ya demokrasia ya nchi zetu za kiafrika, kwamba Chama dola ndicho chenye nafasi kubwa ya kutetea ushindi wake kwenye uchaguzi.
Nafasi aliyokua nayo ni kuitumia nafasi ya kuirudisha heshima yake ya kisiasa kama itapatikana. Kwa bahati nzuri Mungu akamsikiliza kilio chake, nafasi hiyo ikaja.
Tena kutokana na tamaa, yaani tamaa ya pesa na tamaa ya kusimamisha mtu maarufu (siye anayekubalika), ilikua rahisi kwa wanaCHADEMA ambao walihubiri takribani miaka kadhaa kwamba yeye ni fisadi kukubali kumpokea, tena na kumsimamisha kua mgombea wa nafasi ya uraisi kabisa!
EL ndipo alipoona lengo lake limetimia, akagombea akashindwa. Lakini niwaulize swali, je ni mawazo ya watanzania wangapi yamebadilika kutoka kwenye kuamini kwamba Lowassa ni fisadi kwenda kwenye Lowassa ni msafi tena walimsingizia? Jibu ni mawazo ya watu wengi!
Na wingi wa mawazo haya ni kiashiria cha ushindi wa kujisafisha kwa Lowassa, tena kwa kuwatumia wale wale waliomchafua.
Big Up Lowassa, umetumia akili nyingi mno, wewe kweli ni mwanasiasa mzoefu.